Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Ni Wafanyakazi wa kampuni Chloride Exide na walivalia hivyo wakiwa kazini kama sehemu ya maadhimisho ya masuala ya afya kwa wanawake hususani saratani
Walioshiriki walikuwa Wafanyakazi wenye vyeo mbalimbali katika kampuni hiyo akiwemo Afisa Mkuu Mtendaji, Guy Jack
Meneja wa huduma kwa wateja, Stella Kamau amesema wazo hilo liliibuka katika moja ya vikao vilivyokuwa vikijadili shughuli ya kupamba wiki hii ya huduma kwa wateja
Wafanyakazi wa kike ndio waliojitolea mavazi, nguo, viatu na hata mikoba. Pia ndio waliwapodoa Wanaume hao kuhakikisha wanapendeza ipasavyo
Wanaume walifika ofisini wakiwa wamevalia mavazi ya kawaida, lakini wakabadilisha na kuvalia mavazi hayo ya kike
Mbwembwe hizo zilidumu kwa saa kadha lakini kwa baadhi kazi haingetendeka bila mavazi yao ya kawaida, na hivyo walibadilisha baada ya saa kadha.
Lakini kuna wengine waliofurahia sana na kuvalia hivyo kwa kipindi kirefu.
Ingawa shughuli kuu ilifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la viwandani, Nairobi, wafanyakazi katika matawi mengine walishiriki.
"Ofisini palipendeza sana jana. Hata tuna wazo la kuanzisha kundi la mambo ya kufurahisha ambalo litakuwa linatoa mapendekezo ya kipekee ya kufurahisha," anasema Bi Kamau.