Wafanyakazi wa Kiume wa kampuni ya Chloride Exide wavalia kama Wanawake kuadhimisha masuala ya Afya ya Wanawake

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971


Ni Wafanyakazi wa kampuni Chloride Exide na walivalia hivyo wakiwa kazini kama sehemu ya maadhimisho ya masuala ya afya kwa wanawake hususani saratani

Walioshiriki walikuwa Wafanyakazi wenye vyeo mbalimbali katika kampuni hiyo akiwemo Afisa Mkuu Mtendaji, Guy Jack

Meneja wa huduma kwa wateja, Stella Kamau amesema wazo hilo liliibuka katika moja ya vikao vilivyokuwa vikijadili shughuli ya kupamba wiki hii ya huduma kwa wateja

Wafanyakazi wa kike ndio waliojitolea mavazi, nguo, viatu na hata mikoba. Pia ndio waliwapodoa Wanaume hao kuhakikisha wanapendeza ipasavyo

Wanaume walifika ofisini wakiwa wamevalia mavazi ya kawaida, lakini wakabadilisha na kuvalia mavazi hayo ya kike



Mbwembwe hizo zilidumu kwa saa kadha lakini kwa baadhi kazi haingetendeka bila mavazi yao ya kawaida, na hivyo walibadilisha baada ya saa kadha.

Lakini kuna wengine waliofurahia sana na kuvalia hivyo kwa kipindi kirefu.

Ingawa shughuli kuu ilifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la viwandani, Nairobi, wafanyakazi katika matawi mengine walishiriki.



"Ofisini palipendeza sana jana. Hata tuna wazo la kuanzisha kundi la mambo ya kufurahisha ambalo litakuwa linatoa mapendekezo ya kipekee ya kufurahisha," anasema Bi Kamau.
 
Kenya mnatisha.mhh
 
Hapa sasa tuwe makini na wanaume wa wa kenya!
Ukisikia mwanaume wa keny anasema anafanya kazi kiwanda cha betri ujue mvaa gauni huyo!
Wazazi kuweni makini na watoto wenu wa kiume, hasa wanapotafuta ajira waepuke viwanda vya betri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…