PostGE2025 Wafanyakazi wa LHRC waelezea walivyovamiwa Hoteli ya Whitesands

PostGE2025 Wafanyakazi wa LHRC waelezea walivyovamiwa Hoteli ya Whitesands

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Wafanyakazi na wadau wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) waliovamiwa usiku wa jana katika Hoteli ya Whitesands wameeleza hali halisi ya tukio hilo kuanzia lilipotokea hadi leo waliporipoti katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, ofisi ya ZCO, kama walivyoelekezwa kufanya.

Miongoni mwa waliokuwepo ni Deogratius Bwire, Mkurugenzi Ujengaji Uwezo na Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu LHRC; Wakili William Maduhu, Meneja wa Ufuatiliaji wa Uvunjifu wa Haki za Binadamu LHRC; Dkt. Hellen Kijo Bisimba; Wakili Rebecca Gyumi; na Wakili Mariam Magetha kutoka LHRC.
 
Back
Top Bottom