SI KWELI Wafanyakazi wa Marekani wakifanya kazi katika viwanda vilivyorejeshwa na tarrifs

SI KWELI Wafanyakazi wa Marekani wakifanya kazi katika viwanda vilivyorejeshwa na tarrifs

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,
Nimekutana na uzi huu International Forum, unaodai wafanyakazi wa marekani wakifanya kazi katika viwanda vilivyorejeshwa baada ya Tarrifs za Rais Trump.

Screenshot 2025-04-11 100724.png

Je kuna ukweli gani? Video ni ya kweli? Pia, je, ni kweli kazi hizo zinazoonekana videoni zimerejeshwa kama effects za Tarrifs?

Saidia.
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na mvutano wa mataifa makubwa ulimwenguni yakizozana kuhusu kuongezeana ushuru (tarrifs) katika biashara zinazoingia kutoka nje ya mataifa yao. Mvutano mkubwa unaondelea kwa sasa ni kati ya Marekani inayoongozwa na Donald Trump na China.

Madai

Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikinesha baadhi ya watu wenye miili mikubwa (wanene) wakifanya kazi kwenye viwanda. Video hiyo inaambatana na maelezo kuwa hao ni wafanyakazi wa Marekani wanaofanya kazi kwenye viwanda ambavyo vimerejeshwa na ushuru.

Uhalisia

JamiiCheck imefuatlia uhalisia wa madai ya video hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya akili mnemba (AI) kwa ajili ya kufanya propaganda kutokana na mgogoro wa ushuru uliopo kati ya China na Marekani, lengo kubwa likiwa ni kukosoa utawala wa Donald Trump.

Tovuti ya Mirror kupitia makala yake wameandika kuwa mwana TikTok wa kichina alitengeneza kipande hiko cha video kuonesha kwamba kazi zinazoonekana watu hao wakifanya ndizo kazi ambazo Trump anataka kuzirudisha nchini mwake kwa kupandisha ushuru kwa mataifa ya nje yakiwemo China.

Itakumbukwa Aprili 09, 2025, Trump kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Truth alionesha nia yake ya kupandisha ushuru kwa bidhaa za China akilenga ifikie hadi asilimia 125. Trump aliandika;

“Kwa kuzingatia ukosefu wa heshima ambao China imeuonesha kwa Masoko ya Dunia, ninatangaza kuwa kodi ya ushuru (tariff) inayotozwa bidhaa kutoka China na Marekani inaongezwa hadi asilimia 125, na utekelezaji wake unaanza mara moja. Kwa wakati fulani, na tunatumaini kuwa ni hivi karibuni, China itatambua kuwa siku za kuinyonya Marekani na nchi nyingine hazivumiliki tena wala kukubalika.

Kwa upande mwingine, na kwa kuzingatia kuwa zaidi ya nchi 75 zimewasiliana na Wawakilishi wa Marekani, zikiwemo Wizara ya Biashara, Hazina, na Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani (USTR), ili kujadili suluhisho kuhusu masuala ya Biashara, Vizingiti vya Biashara, Ushuru, Udhibiti wa Sarafu, na Ushuru Usio wa Kifedha—na kwamba nchi hizi hazijachukua hatua yoyote ya kulipiza kisasi dhidi ya Marekani, kama nilivyoshauri kwa nguvu—nimeruhusu kusitishwa kwa siku 90 (PAUSE), na kupunguzwa kwa kiwango cha ushuru wa biashara wa mabadilishano (Reciprocal Tariff) hadi asilimia 10, ambacho kitaanza kutumika mara moja.

Asanteni kwa kulipa uzito suala hili!”
Back
Top Bottom