mkweliwatz
Member
- Dec 6, 2025
- 8
- 11
Sisi Wafanyakazi 160 tuliopo katika Mgodi mdogo ambao unapatikana Mkoani Mara, Wilaya ya Musoma, Kata ya Kigera, Kijiji cha Kwitope chini ya Kampuni ya IDERA au GDM tuna changamoto ambazo tunatamani jamii izisikie na ujumbe ufika kwa mamlaka husika ili utatuzi upatikane.
Tunacheleweshewa sana mishahara na kibaya zaidi tunafanyakazi tukiwa hatuna mikataba ya ajira, mara mojamoja wanatoa mikataba ya miezi mitatu-mitatu, hatuna Bima ya Afya na kwa ufupi tunaishi kama Watumwa au tupo utumwani.
Maafisa wa Serikali wakija kukagua wanapewa ‘mzigo’ wanaondoka wakiwa hawajafanya chochote, na hata kutusikiliza Wafanyakazi hawafanyi hivyo, wao wanazungumza na viongozi wa juu kisha wanaondoka.
Tunaomba ujumbe huu ufike kwa Waziri wa Madini, tumejaribu kutafuta haki katika ofisi nyingi za Musoma hatujapata haki yetu kwa kuwa mabosi wetu wanatamba kuwa wameiteka Serikali na hawawezi kufanywa chochote.
Tunateseka sana, mfano mshahara wa Januari 2026 tumekuja kupewa Februari 17, 2026 na ikitokea ukahoji unajibiwa kibabe kwamba “Kama hutaki kazi ondoka, na nenda kokote unapotaka kashtaki”.
Kuna dada ambaye ndiye msimamizi wa wafanyakazi, amekuwa akitumia kauli za konesha kwamba wao hawawezi kufanywa chochote.
Tulifikisha malalamiko yetu mara kadhaa kwa TUICO (Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri) hapa Musoma, lakini alikuwa anatupuuza n hata ilipotokea mwakilishi wao amekuja, aliishia kufanya kile wanachokifanya wenzake wa Serikalini kuondoka.
Afisa wa TUICO alichotuambia ni kuwa Kampuni yetu tunayoifanyia kazi imesajiliwa kama Kampuni ya Ujenzi lakini sisi tunajihusisha na kuchimba madini, ndio maana hata aina ya mikataba wanayopewa inakuwa na ujanjaujanja mwingi, pia wanaopewa mkataba hakuna sehemu inayoandikwa utalipwa sh ngapi, sasa hapo inaonesha jamaa wanajua kucheza na akili za maafisa wa Serikali.
Serikali itusaidie kwani tunaoumia ni sisi Watanzania ambao maisha yetu ni duni na wanajua hatuna cha kuwafanya.