Wafanyakazi wa New Sideway Bar Bunju, Dar es Salaam jirekebisheni mnafukuza wateja

Waajiri wote wanaotoa huduma za kijamii wapeleke watoa huduma wao katika kozi fupi za Customer Care.Ikibidi baada ya kuajiri wapite kwenye hizo kozi kwanza kabla ya kuanza kazi.
Wahudumu wa ndege ni mfano wa fani zinazotumia mtindo huu wa kuwapeleka kwenye kozi mbali mbali ikiwepo customer care .
Tanzania waajiriwa wengi sio wote wanadhani kwamba wanawafanyia favor wateja.Ndio maana wengi wanadengua na kudai tip.
 
Ni kwa masikitiko kuwa wafanyakazi wa Baa ya New Sideway iliyoko Bunju A Kinondoni DSM hasa wanaohudumia vinywaji wamekuwa na tabia mbaya sana ya ubaguzi katika kuwahudumia wateja.

Kama wewe hutoi offer au huna urafiki na wahudumu jua imekula kwako. Unaweza kufika unakaa unasubiri mhudumu akusikilize haji na unawaona wapo tu karibu wamekaa makundi makundi wakipiga soga ila cha kushangaza akija mshikaji wao wataamka fasta kumkimbilia na kwenda kumsikiliza. Inakubidi usubiri au uite kwa kulazimisha ndo atakuja kukusikiliza na akishakuhudumia anapotea jumla kwenda kukaa na washkaji wao.

Ukweli ni kuwa wahudumu wa hii baa ni wapuuzi wakubwa hawajielewi na wataua hii baa muda si mrefu, watu wengi hawaridhishwi na tabia hizi wanaenda tu kwa vile hakuna namna ila endapo patatokea Bar mbadala basi wajiandae kufa kifo cha mende.

Nimehama rasmi hii baa nakunywa zangu maeneo ya Boko, au Tegeta au Mbezi.

Najua watajitetea ni wivu au vita za kibiashara ila huo ndo ukweli. Meneja naye hajielewi kabisa kwanza anawaogopa wahudumu.

Ni hayo tu
Vichwa vinafikiria jinsi ya kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla pamoja na kuepukana na Omicron we akili ipo kwenye pombe na bar waitress?
 
Hao wahudumu itakuwa walipelekwa kozi fupi Arusha,maana wahudumu wengi wa mabaa na mahoteli arusha wanaweza hata kukutukana ikiwa utaendelea kuwaita wakuhudumie wakati ama anaongea na simu,anaongea na shogaake,au anafumua nywele zake,kuhusu huduma mbaya kwa wateja usisite kutembelea arusha,utaniheshimu baadae.
 
hahaaaa kweli bia tamu.....hamia River Wood Bunju B .. ama vuka daraja la bagamoyoo kuna viwanja vya kujinafasi kama Kimele Resort au Ndoto Pole Pole (hapa lazima ufanye booking)

.. Meneja naye hajielewi kabisa kwanza anawaogopa wahudumu.....meneja amelewa huduma ile ya baadae ya wahudumuuu

mbona vijiwe viko vingi sanaa we unakariri sehemu moja tuuuu .... ka una kifua vuka nenda apo jirani pana Posto Bella Garden yenye had swiming pool .... ama kula akapulco mbweni ... ama njoo huku kwetu Gobaaa
Posto iko bunju gani

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Na Wewe jifunze kutoa tip uone watakavyokuchangamkia. Sio unahudumiwa vizuri tu alafu unaondoka hata huachi tip mezani
 
Madem wengi wa Bar Ni wauza k tu pale wamenificha Kama wahudumu Ila sicho kilichowapeleka pale .Bahat mbaya mameneja wengi hawalijui hili wao wanaangalia mauzo tu ,ndio maana bar nyingi zinakufaga kifo Cha mende endapo itafunguliwa mpya jirani na hapo.

Madem wa bar hawawez kukuchangamkia km utaenda na sweet wako lazima watanuna ,Kama huwapi offer na kibaya Zaid wanaambizana kabisa kua yule Ni mtoaj mzur wa offer yule Ni bahili.

Jiulize umetoka home kwako na bajet yako ya kunywa et uwatengee na mabarmed bajet ya kuwafurahisha ,upuuuz huu.
 
Ni kwa masikitiko kuwa wafanyakazi wa Baa ya New Sideway iliyoko Bunju A Kinondoni DSM hasa wanaohudumia vinywaji wamekuwa na tabia mbaya sana ya ubaguzi katika kuwahudumia wateja.

Kama wewe hutoi offer au huna urafiki na wahudumu jua imekula kwako. Unaweza kufika unakaa unasubiri mhudumu akusikilize haji na unawaona wapo tu karibu wamekaa makundi makundi wakipiga soga ila cha kushangaza akija mshikaji wao wataamka fasta kumkimbilia na kwenda kumsikiliza. Inakubidi usubiri au uite kwa kulazimisha ndo atakuja kukusikiliza na akishakuhudumia anapotea jumla kwenda kukaa na washkaji wao.

Ukweli ni kuwa wahudumu wa hii baa ni wapuuzi wakubwa hawajielewi na wataua hii baa muda si mrefu, watu wengi hawaridhishwi na tabia hizi wanaenda tu kwa vile hakuna namna ila endapo patatokea Bar mbadala basi wajiandae kufa kifo cha mende.

Nimehama rasmi hii baa nakunywa zangu maeneo ya Boko, au Tegeta au Mbezi.

Najua watajitetea ni wivu au vita za kibiashara ila huo ndo ukweli. Meneja naye hajielewi kabisa kwanza anawaogopa wahudumu.

Ni hayo tu
Acha ulevi
 
Wahudumu wengi wajinga hasa wadada huchangamka meza ikiwa na waume wakija wanawake hununa na ukiondoka kidogo wanajichekesha na kuja, in short tanzania kwa customer care ni sifuri

Bado hawajakimbia na kujizungusha na chenji, au kuongeza bei ya vinywaji.
 
Bia tamu na mteja ni mfalme.. Kwanini huko nako wakuchanganye ubongo? Hama fasta.. Nenda mahali ambako ukifika tu getini unapokelewa na mnyange mwenye shanga zake kiunoni na tabasamu la kumtoa nyoka pangoni
Hiyo Hali ya kupokelewa Kama mfalme inabidi uitengeneze.
Kuna sehemu nilikwenda bar, akaja maid mmoja nikamuagiza akaniletee kongoro na yeye achukue lake Kama anataka. Baada ya kongorro nikamwambie aniletee castle lite baridi na yeye achukue kinywaji anachotaka. Akachukua msengerema lite, nikaagiza ya pili na yeye nikamwambia naye aongeze yake. Tulienda hivyo mpaka bia ya nne. Akaleta bili zote nikalipa zile coin nikamwambia Ni nauli yake. Ile nawasha gari niondoke namwona huyu. Namuuliza Kuna kitu sijalipa akasema la hasha. Sasa kunani ? Akasema hujachukua namba yangu. Nikamwambia asikonde kesho nitakuja.
Kesho yake nilipokelewa Kama mfalme halafu mchezo ukawa Ni ule ule Ila niliagiza kuku choma mzima ili tule wote.
Siku ya tatu nilimkuta ametoka kidogo hivyo nikahudumiwa na mwingine, siku hiyo niliagiza supu ya samaki. Yule wa siku ya kwanza alivyorudi alikoenda alikuta mezani kwangu tayari Yuko mwenzie anakula supu ya samaki na castle lager na mishkaki miwili pembeni. Aisee alimkata mla samaki jicho sio la kawaida.
Basi kwenye Ile bar kila nikienda napokewa Kama Bashite enzi za mwendazake.
 
Ni kwa masikitiko kuwa wafanyakazi wa Baa ya New Sideway iliyoko Bunju A Kinondoni DSM hasa wanaohudumia vinywaji wamekuwa na tabia mbaya sana ya ubaguzi katika kuwahudumia wateja.

Kama wewe hutoi offer au huna urafiki na wahudumu jua imekula kwako. Unaweza kufika unakaa unasubiri mhudumu akusikilize haji na unawaona wapo tu karibu wamekaa makundi makundi wakipiga soga ila cha kushangaza akija mshikaji wao wataamka fasta kumkimbilia na kwenda kumsikiliza. Inakubidi usubiri au uite kwa kulazimisha ndo atakuja kukusikiliza na akishakuhudumia anapotea jumla kwenda kukaa na washkaji wao.

Ukweli ni kuwa wahudumu wa hii baa ni wapuuzi wakubwa hawajielewi na wataua hii baa muda si mrefu, watu wengi hawaridhishwi na tabia hizi wanaenda tu kwa vile hakuna namna ila endapo patatokea Bar mbadala basi wajiandae kufa kifo cha mende.

Nimehama rasmi hii baa nakunywa zangu maeneo ya Boko, au Tegeta au Mbezi.

Najua watajitetea ni wivu au vita za kibiashara ila huo ndo ukweli. Meneja naye hajielewi kabisa kwanza anawaogopa wahudumu.

Ni hayo tu
Hili ni tatzo kubwa sana la wahudumu.
Kuna siku niliingia shooters mtwara, wahudumu wameuchuna tu, nikamtafuta mhudumu mmoja mrembo, nikamuuliza mbona sisikilizwi au sababu sijaning'iniza funguo za gari?
Dah alijishtukia, ananihudumia mpaka na mengine, kifup bar nging zinakufa sababu ya huduma/wahudumu
 
Wahudumu wengi wajinga hasa wadada huchangamka meza ikiwa na waume wakija wanawake hununa na ukiondoka kidogo wanajichekesha na kuja, in short tanzania kwa customer care ni sifuri
Nadhani kabla nchi haijapiga hatua tuwekeze katika kujali wateja, wateja ni muhimu kuliko biashara zetu maana bila wao twazifunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi exposure ndogo sana wallah Kuna sehemu ukienda kwa huduma zao unakuwa mteja permanent Sasa shida watu wamepata tu hela na kuanzisha biashara na kusahau kuhusu huduma kwa wateja
 
Ndo maana mimi nikiingia bar natafuta kaunta iko wapi, napenda sana kuhudumiwa na mhudumu wa kaunta halafu walio wengi wanajielewa
 
Kwani hakuna meneja wa bar hapo? Tatizo wa Swahili hatujui kutoa huduma kwa Wateja na kuwasikiliza wa teja tatizo lina anzia kwa uongoz kuto wajari wafanyakaz na kuangalia mauzo tu, na kuto fatilia utendaji wa staff
Meneja au mwenye baa kala wahudumu ndiyo maana hawawezi kuwaongoza......halafu uwe unawanunulia hata mbili tatu then unakuwa mfalme ghafla
 
Ni kwa masikitiko kuwa wafanyakazi wa Baa ya New Sideway iliyoko Bunju A Kinondoni DSM hasa wanaohudumia vinywaji wamekuwa na tabia mbaya sana ya ubaguzi katika kuwahudumia wateja.

Kama wewe hutoi offer au huna urafiki na wahudumu jua imekula kwako. Unaweza kufika unakaa unasubiri mhudumu akusikilize haji na unawaona wapo tu karibu wamekaa makundi makundi wakipiga soga ila cha kushangaza akija mshikaji wao wataamka fasta kumkimbilia na kwenda kumsikiliza. Inakubidi usubiri au uite kwa kulazimisha ndo atakuja kukusikiliza na akishakuhudumia anapotea jumla kwenda kukaa na washkaji wao.

Ukweli ni kuwa wahudumu wa hii baa ni wapuuzi wakubwa hawajielewi na wataua hii baa muda si mrefu, watu wengi hawaridhishwi na tabia hizi wanaenda tu kwa vile hakuna namna ila endapo patatokea Bar mbadala basi wajiandae kufa kifo cha mende.

Nimehama rasmi hii baa nakunywa zangu maeneo ya Boko, au Tegeta au Mbezi.

Najua watajitetea ni wivu au vita za kibiashara ila huo ndo ukweli. Meneja naye hajielewi kabisa kwanza anawaogopa wahudumu.

Ni hayo tu

Mimi hawa nimewakomesha sana hasa kule Sinza. Nilikuwa nikiwasubiri hadi kufokeana nilichokuwa nafanya kwa hadira ni kuagiza pia nyama! Nikishaletewa basi naendelea kula nyama na kunywa kinywaji. Ilishafika muda wa kuomba maji ya kunawa nilikuwa napiga kinywaji fasta na kukimaliza, halafu natega macho jikoni kuangalia aliyeniletea nyama yupo busy na mteja gani wa kuagiza nyama au anapeleka nyama wapi! Nikishagundua yupo busy au anamprlejea nyama mteja mwingine hapo ndipo mimi nilikuwa nachomoka kama kenge bila hata kunawa! Nilikuwa naenda kunawa bar nyingine huko nilikoelekea! Nimekomesha bar karibu zote pale Sinza, na nilikuwa sirudi kwenye hizo bar kwa muda wa miezi mingi hadi wasahau. Kuna mchoma nyama mmoja siku moja akaninasa kwenye bar yao, alinifuata na kuniambia ‘ wewe bwana kuna siku ulikula nyama na ukaondoka bila kulipa’. Nikamjibu kuwa hapa wachoma nyama mpo wengi na mimi nilimpa hela mwenzenu mmojawapo. Akaondoka huku ameguna! Sasa bar nyingi pale Sinza nikiagiza nyama huwa wapo macho sana wanafuatilia hadi ninapomaliza kipande cha mwisho cha nyama na fasta utakuta wamefika na maji ya kunawa. Ukishamaliza kunawa hapo hapo wanataka na hela maana wanajua kitendo cha kugeuka na kuelekea jikoni bila hela watashangaa na mimi huku nyuma nimeyeya chap chap!
 
Back
Top Bottom