Mtanisamehe, mimi niko tofauti na wengi najua, pls mnivumilie.
Kinachoniudhi siku zote ni pale mtu anaposaini mkataba mwenyewe na baadae hautaki tena, hivi inakuwaje? ni mara baada ya kuona watu wanavyokuja na cash kununua vitu vingi na wao wanatamani? au ni kweli mishahara waliokubaliwa/waliokubaliana hawapewi?
Je kama pobation inakwisha baada baada ya performance yako kuridhisha, kuna upimaji uliowazi wa kuwapima kama wanastahili kuajiriwa au bado waendelee kujaribiwa?
Kubwa linalonitatiza ni jinsi walivyo wezi. Wasichana wadogo lakini wezi ajabu!!!
Hawakujui ila ukienda wanakuomba ulipe kidogo (pungufu ya bei halisi) ili usipewe risiti!
Au wanakuletea nje kabisa!
Usipokuwa mwangalifu baadhi ya vitu ulivyochukua hawaweki kwenye risiti kabisaaaa!
Wakiajiriwa wanakuwa kawaida kabisa, wakikaa mwezi, wameshanunua dhahabu, na kila aina ya perfume.
Kweli kukaa na kuona vitu vizuri kila siku kunatia vishawishi, ila ndo ukubali kupoteza kazi unapoiba ukikamatwa.
Wanajidhalilisha wenyewe kwa kuiba kila kitu, mwajiri atawaheshimu vipi? Wanategea kazi kila wakipata upenyo, kama watoto wa chekechea.
Lazima wajue kuwa kazi ya kuuza shoprite haina/haitakiwi kuwa na hadhi tofauti na kuuza kwenye fremu huko mtaani, ni kuuza duka tu, wanataka walipwe kama manesi?? au walimu?