Wafanyakazi wa viwandani angalau kesho lisemwe neno juu yao nao ni watanzania wenzetu

Wafanyakazi wa viwandani angalau kesho lisemwe neno juu yao nao ni watanzania wenzetu

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
2,944
Reaction score
2,032
Naandika haya kwa hisia nyingi sana baada ya kupita pita huko na huko kutafuta riziki maana imeandikwa asiye fanya kazi na asile.

Mwaka fulani nilishawahi kujikuta naangia huko viwandani kutafuta chochote kitu kusema ukweli ukiacha hawa waliajiriwa viwandani kuna hili kundi linaloitwa vibarua japo utakuta mtu hapo kiwandani, Ana miaka 3 au zaidi yani ni "KIBARUA SUGU".

Maisha ya huyu kibarua sugu hawa wamiliki wa viwanda wanachofanya kukwepa kumuajiri ni kumpumzisha kill baada ya miezi mitatu na kumrudisha tena kazini kama muajiriwa mpya ili mradi tu asiwe na haki ya kuajiriwa lakini ukifatilia kwa undani utakuta mtu huyu ni muhimu sana kwa mwenye kiwanda ila kwa kuwa anao uhuru wa kuwachezea watanzania hawa basi anawatumia kwa kuwakandamiza.

Unakuta hawa maboss wa viwanda wanadhamini hadi team za mpira lakini malipo anayolipwa kibarua sugu yanasikitisha na hamna anayejari walau kuwashawishi maboss hawa angalau kuongeza kiwango cha ulipaji zaidi ya wao kujipa faida kubwa.

Kuna mengi sana huko viwandani baadhi ya viwanda mfanyakazi anakatwa hela kuchangia staff bus ambalo ni jambo la ajabu sijawahi ona popote hapa Duniani, maskini huyu ambaye kipato chake tu chenyewe hakitoshi kusukuma hata wiki 2.

Kweli tunawathamini wawekezaji lakini natamani kesho lisemwe neno lakutia matumaini juu ya kundi hili la watanzania wenzetu ambao kamba yao himo humo viwandani.
 
Inasikitisha sana ndugu,tuko kwe nye modern slave era.WATANZANIA WA HALI YA CHINI HAWANA TOFAUTI NA WATUMWA na hakuna anayejali
 
Ni kweli una hoja yenye mashiko, lakini sidhani kama hoja hii ina Mtu sahihi wa kuisemea huko ulikoielekeza.
Hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkuu ndio wakuongea,maana wabunge wako kimya lakini wangekuwa wana ndugu huko viwandani labda ingewauma wangeongea
 
Back
Top Bottom