jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Wanajamvi, Leo nimesikiliza madam President Samia Suluhu Hassan mwanzo mwisho. Mimi siyo mfanyakazi, lakini niliikubali hotuba yake na kuona busara nyingi sana ndani yake.
Hata hivyo, sikuwa najuwa wafanyakazi wenyewe wameipokeaje hotuba hiyo. Jibu nililipata mtaani.
Kwa kifupi sana, wafanyakazi leo wamekula bata mbaya kabisa. Wakiwa wenye furaha na matumaini.
Siyo tu matendo yao yalionyesha hayo, bali hata nyuso zao. Sikuamini mimi mwenyewe nikaanza kuwauliza maswali kiudadisi tu. Walinihakikishia kuwa furaha yao imetokana na hatua za mama kwenye hotuba ile! Nilishangazwa na uelewa wao! Nikajuwa nao wakiona kama mimi nilivyoona!
Pamoja na kwamba hawakuongezewa mishahara, lakini hatua alizochukuwa kama mfano punguzo la PAYE kwa asilimia moja, malipo ya deni la mikopo ya vyuo kwa asilimia sita pamoja na utegemezi wa bima kutoka miaka 18 hadi 21, ni zaidi hata ya nyongeza za mishahara.
Na ukizingatia kwamba ameahidi kuanzia mwaka ujao kufanya hayo, basi amewakhosha haswa wafanyakazi siku ya leo. Hata mimi nilifurahi sana kuona furaha zao!
Kitu pekee cha kuhofia, ni hofu yenyewe. Mama yuko vizuri.