Wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kuliko wafanya biashara

Hustler1

Senior Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
116
Reaction score
111
Amini amini nakwambia mfanyakazi mwenye mshara wa 2M kwa mwezi kodi yake haipungui 3M kwa mwaka

Amini amini tena nakwambia mfanya bishara mwenye mtaji unaompa faida ya 2M kwa mwezi kodi yake haizidi 400k kwa mwaka.

''The income from your 5-9 job is taxed at a higher rate than any other form
of income''.

Over.
 
Mimi kila mwezi wanakula laki mbili na 30! Ukizidisha mara 12, ndipo utakapogundua wafanyakazi wa nchi hii cha moto tunakiona.
 
Pitia vzuri hapa kabla ya kufikia conclusion


Unajua mauzo ya milion 5 kwa mwaka ninfaida ya shingi ngapi? Halafu fanya malinganisho na huyo mfanyakaz unayesema analipa kodi kubwa


Pili, kodi ya mfanyabiashara ndo inalipa salary
 
Mimi kila mwezi wanakula laki mbili na 30! Ukizidisha mara 12, ndipo utakapogundua wafanyakazi wa nchi hii cha moto tunakiona.
Kawaida wafanyakazi huwa hatuhesabu mshahara as a basic,,,, tunahesabu ile take it to home baada ya hayo makato yao huo ndio mshahara

Me huwa inaniuma ile hela nayokatwa kuchangia chama na wakati hakinisaidii chochote,, ila mambo ya tax walaa
 
Mimi kila mwezi wanakula laki mbili na 30! Ukizidisha mara 12, ndipo utakapogundua wafanyakazi wa nchi hii cha moto tunakiona.
Kawaida wafanyakazi huwa hatuhesabu mshahara as a basic,,,, tunahesabu ile take it to home baada ya hayo makato yao huo ndio mshahara

Me huwa inaniuma ile hela nayokatwa kuchangia chama na wakati hakinisaidii chochote,, ila mambo ya tax walaa
 
Rafiki ni biashara ipi hiyo inayotengeneza 2,000,000/=kwa mwezi na kodi yake aizidi 400,000/=acha kazi ufanye hiyo biashara.Ukiacha biashara za magumashi,ukiona biashara halali inatengeneza faida ya 2,000,000/=ujue mtaji na uwekezaji waki ni mkubwa
 
Acheni kazi mjiajiri kama sisi tunafaidi.
 


wafanyabishara ni wengi kuliko wafanyakazi hilo la kulipa salary wala sio issue.
 
Nafikiri unaongea usichokifahamu. Mfano mmoja nakupa. Biashara iliosajiliwa kama kampuni inatakiwa ilipe kodi 30% ya faida yake. Hii ni mbali na VAT,PAYE etc. Sasa turudi kwenye faida ya 2m kwa mwaka ni 24m sasa hapo inabidi ulipe kodi 30% ambayo ni 7.2m....hapo vipi?
 
Hakuna mfanyabiashara anayepata faida ya 24m kwa Mwaka akalipa kodi 7.2m kwa Mwaka! Akilipa 7.2m kwa Mwaka kama kodi ujue kapata faida ya zaidi ya 100m kwa Mwaka husika. Mfanyabiashara anategemewa na TRA kutoa information za mauzo ndio AKADIRIWE kodi! Wengi huwa wanatoa false information kukwepa kodi! Hakuna mfanyakazi anayekadiriwa kodi, huwa wanalipa exactly wanachotakiwa kulipa kwa sababu system za mishahara yao ziko well controlled. Kama wafanyabiashara mauzo yao yangekuwa yanapita kwenye channel Fulani ambayo gvt unaweza kuona tungekuwa tunakusanya trillion 3+ kwa mwezi! (Achana na EFD receipts kwani wengi hawakati)
 

Duniani kote ndio hali ilivyo. Na ndio maana watu smart hawakubali kuajiriwa (unless ni kwa lengo la kujifunza practically ABC za profession waliyoilenga). Ni wachache wanaokuwa mamilionea kutokana na kuajiriwa.
 
Sijawahi kuona milionea ambaye ni mtumishi wa Uma. Mtumishi wa umma ni mwoga wa maisha akifikisha miaka 50.
 
Nafikiri umerukia tu nakujibu bila kujua chimbuko la post yangu. Mleta mada KASEMA 2M PROFIT PER MONTH. Na mimi nimemjibu hesabu ya kodi ya profit ya 2m per month in a year. Whether wafanyabiazhara wanalipa kodi au hawalipi makuachia wewe to judge coz you seem to know all businessmen in Tanzania.
 
Kama hujanielewa vzr hapo juu basi siwez kutumia nguvu zaidi
 
Acha kazi ,ufanye biashara uone kimbembr chake
 
Acha kazi ,ufanye biashara uone kimbembr chake
Mi nimeongelea kodi, swala LA biashara imekuwa ngumu/rahisi hayo ni mambo mengine.
Hoja ni kwamba employee makato ni makubwa sana ukilinganisha na kipato chao.
Kingine failure no 1 kwenye biashara ni kufuata sheria zote ikiwemo kulipa kodi 100%.
 
Hili jibu linamfaa sana, aache kazi afanye biashara kama hajafunga ndani ya mwezi[emoji3][emoji3]

Anajiskia raha kukunja kila mwez hela ambayo anatafutiwa na mfanyabiashara
Acha kazi ,ufanye biashara uone kimbembr chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…