Wafanyakazi wanne wa vyombo vya habari watiwa nguvuni Tigray - Ethiopia bila kuambiwa sababu ya kukamatwa kwao

Wafanyakazi wanne wa vyombo vya habari watiwa nguvuni Tigray - Ethiopia bila kuambiwa sababu ya kukamatwa kwao

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Wafanyakazi wanne wa vyombo vya habari wamekamatwa na vyombo vya usalama katika eneo lililokuwa na mapigano la Tigray nchini Ethiopia.

Tangu kuzuka kwa mapigano mwezi Novemba mwaka jana baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia kutangaza hatua za kijeshi dhidi ya kundi la TPLF akiwashutumu kuvamia vikosi vya jeshi, kumekuwa na vizuizi dhidi ya vyombo vya habari kuwepo katika eneo hilo na kukusanya taarifa kwa uhuru.

Hadi sasa, ni vyombo saba tu vya habari vya kimataifa ndivyo vimepewa kibali cha kufanya kazi katika eneo hilo, vikiwamo AFP, BBC na Financial Times ambavyo wafanyakazi wake ndio wametiwa kizuizini.

Hata hivyo, vyombo hivyo vilipewa onyo la mapema kuwa wafanyakazi wake wanaweza wakakumbwa na 'njia za maelekezo' ambazo hazikuwekwa wazi, kama hawatakubaliana na viwango vilivyowekwa na serikali ya eneo husika.

Waliokamatwa ni watafsiri waliokuwa wakifanya kazi na waandishi wa habari wa AFP na Financial Times siku ya Jumamosi, huku Shirika la Utangazaji la Uingereza likisema kuwa mwandishi wake wa habari naye ametiwa nguvuni. Baadhi ya wafanyakazi hao wanashikiliwa katika chuo cha kijeshi karibu na mji wa Makele.

Kiongozi wa Serikali ya Mpito katika eneo hilo hakuweka wazi ni kwa nini wamekamatwa lakini amesema kuwa wapo chini ya uchunguzi na kuwa kuna ushahidi ambao umeshapatikana bila kuweka wazi ni ushahidi gani.

Financial Times imesema inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa wafanyakazi wake wanaachiwa, huku Shirika la Utangazaji la Uingereza likieleza kuwa limefikisha malalamiko yake kwa uongozi wa Ethiopia na linasubiri majibu. Kitendo cha kukamatwa kwa wafanyakazi hao kimelaumiwa na asasi inayotetea uhuru wa habari duniani, Committee to Protect Journalists (CPJ) ikisema kuwa kitendo hicho kitaongeza woga kwa waandishi wengine kufanya kazi katika eneo hilo.

Chanzo: AFP
 
Back
Top Bottom