Wafanyakazi watakaokataa kujiunga na DP World watapelekwa kufanya kazi bandari nyingine. Je, TPA wamekabidhi bandari yote Dar kwa DPW?

Mkuu lazima tukubali kwamba sisi kuendesha tumeshindwa. Na kushindwa kwetu kunachangiwa na sisi wenyewe kukosa uzalendo wa kusimamia rasilimali tulizo nazo.pili mwekezaji anakuja na teknolojia na fedha of which si kama tungeshindwa lakini tatizo sisi wenyewe bado hatupo tayari.
 
Kumbe unayajua haya mkuu..kwa vile tumeshindwa kujisimamia, wacha tusimamiwe na na wageni. Hii ndio point yangu ya msingi. Tuliwaamini watu waendeshe bandari yetu kizalendo..Sasa wameshindwa..so wana uchaguzi wa ama kuwa chini ya wageni ama kuhamia kwenye hivyo vibandari vingine.
 
Wanataka kuwafukuza wazawa wote ili wabaki peke yao wapate nafasi ya kupitisha silaha na dawa za kukevya. Rais Samia naye awaachie ikulu hawa waarabu wake ahamie nchi nyingine.
 
Hivi unajisikia unacho kiongea!?
Serikali ya ccm ijaze makada ishindwe kuindesha bandari iseme watanzania wote wameshindwa kuendesha bandari
 
Wabongo banaaaa!!!! Unafurahia anguko la mwenzako ?
Unapata faida gani mwenzio akifukuzwa kazi
Kwani kuingia sector binafsi ni kufurahia kufukuzwa kazi?

Huku sekta binafsi kitakachokubeba ni utendaji wako wa kazi na uwajibikaji ndicho kitu watu wengi wa serikalini ndio wanakiogopa na hawakitaki kabisaa, ukweli ni huo waajiriwa wengi wa serikalini hawana uwajibikaji sawa sawa kwenye majukumu yao wala sio unafiki na uchawi wa watu tunaosema mnaingia sekta binafsi ikiwa unataka kukaa hapo bandari salama.

Kama hakukufai basi uende huko mamlaka inapoona patawafaa wala sio kesi ili muendelee kubweteka na ajira za kudumu.

Kwenye hili la uwajibikaji mie naona sawa watumishi wengi wa serikalini wapewe kazi za mikataba ili ukizingua waje wengine tofauti na sasa unakuta mtu anaubabaifu mwingi halafu wala haoni aibu kisa tuu ni mwajiriwa wa kudumu.

Fikra hizi ndio zinatukwamisha kwa maendeleo ya nchi yetu na watu kuwa wavivu kupindukia.
 
Sasa mnaingia private sector, yale mazoea ya ajira ya kudumu myatoe kichwani na uwajibikaji ndio sera za private, ila mnaweza kwenda TPA mbambabay au Kigoma huko.

Sasa mnaingia private sector, yale mazoea ya ajira ya kudumu myatoe kichwani na uwajibikaji ndio sera za private, ila mnaweza kwenda TPA mbambabay au Kigoma huko.
kuongezea tu private sector ina run on performance, wanaingia kwenye ushindani. Kama wamezoea kufanya kazi kivivu itawa cost
 
Bandari na DP wamegawana maeneo si gati zote. For the record wananchi wa tz most of time tukipewa mashirika huwa tunazingua? Bandari tumeiendesha for how many years?

Outcomes ilikuwa nini?

Sometimes serikali inaona bora impe mwekezaji sababu mbongo ana bad track record (si mashirika yote) kwenye ku run critical business kama hizi
 
Hivi unajisikia unacho kiongea!?
Serikali ya ccm ijaze makada ishindwe kuindesha bandari iseme watanzania wote wameshindwa kuendesha bandari
Hap makada wanatoka mbinguni? si wanatoka kwenye jamii yetu na ndio watanzania hao hao?

Bottom line huwez mpa kila mtanzania nafasi ya ku run bandari. Under mfumi ule ule hata akija mtz kutoka nje, atazingua tu at some point.
watanzania tume run bandari wenyewe for how many years? Nini tulifaidika kama nchi?
 
Mbona unauliza majibu ?
 
Porojo kibao ! kwanini usijibu swali alilouliza mleta uzi ?
 
Tupo pamoja
 
Wezi ni management ya TPA au wafanyakazi wote1!?
Au watanzania wote kuanzia raisal mpaka mfagizi
 
Wezi ni management ya TPA au wafanyakazi wote1!?
Au watanzania wote kuanzia raisal mpaka mfagizi
who knows ni management au wafanyakazi? Mara ngapi jpm kabadilisha management ya badnari and then madudu yaliendelea?

Hii kitu ni chain ndefu sana from top to bottom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…