Wafanyakazi wengi wa Serikali wanaishi maisha artificial ndio maana wanaona mishahara haitoshi

Wafanyakazi wengi wa Serikali wanaishi maisha artificial ndio maana wanaona mishahara haitoshi

Mkuu unapokua unafanya kazi serikalini kwenye swala la mkopo kuna kitu kinaitwa 1/3 kwaio kimsingi huwezi kukopa kupitiliza hio 1/3 ya mshahara kwaio kama mshahara 700000÷3 = 233,000 kwaio utakopa ukopavyo hio senti itabaki kunako account ya mshahara...Wapi Mark X tujaze full tank wikend imeshaingia...
 
Acha kupangia watu maisha mtu akiona mshahara haumtoshi ataamua mwenyewe kuacha au kuendelea.
 
Wafanyakazi wengi wa serikali wanaishi maisha artificial ndio maana wanaona mishahara haitoshi.

Unakuta mtu ana mshahara laki saba kakopa benki kanunua gari na zingine anajenga bonge la jumba.

Hela ikiingia benki wanakata anabaki na laki moja!!! Anaanza kuishi kwenye mzunguko wa madeni kopa huku nk.

Wafanyakazi wengi wanejaa madeni ya kijinga jinga tu heri wangekopa na kuwekeza lakini mikopo mingi ni ya ku finance artificial life style isiyoendana na kipato halisia.
dunia nzima middle class ina mikopo ndio mana kama africa hawataki kuitoa serikali iliyoko madarakani kwasababu ikitoka hawajui future itakuwaje na wata services vp mikopo yao
 
Mtoa mada wasipojenga ili kuepuka kodi na waaiponumua gari ili kupata ya kwendea na kurudi kazini wangefanya nini?uekezaji au biashara ni nani ataisimamia???angalizo usije ukakopa halafu ukafanya biashara na kuwaachia eti wadogo zako ndio wasimamie.au mtu wa mbali asiekuwa na uchungu na hela ulioekeza asimamie.baba utakufa kwa presha na kuzikwa na huku unadaiwa.
Angalau mtu ajenge nyumba na kupangisha atapata hela nyingi kuliko anayokatwa huko banki kwa mwezi.
Au afanye biashara lkn msimamizi awe ni mke wake kama na yeye anauwezo huo wa kuendeleza biahara .maana wake zetu nao wana mambo mengi
 
Itasikitisha sana, endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...
 
Shida iko wapi? Kama akija kwako kukopa mwambie ila Kama hajawai kuja kwako mwache! Kila mtu ashinde mechi zake! We kopa fanya biashara, yeye akope anunue gari na nyumba kubwa, MAISHA YAENDELEE!!!!!!!
 
Back
Top Bottom