Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 26 kwa tuhuma za biashara haramu ya upatu mtandaoni bila kibali cha BoT, wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Leo Burnett London (LBL) na mkurugenzi wao, Najim Houmud.
Watuhumiwa hao walikamatwa kati ya Februari 18 hadi 22, 2025, na kufanya idadi yao kufikia 38 baada ya wengine 12 kukamatwa Morogoro na Mbeya. Kampuni hiyo inadaiwa kuwatoza wanachama Sh50,000 kama ada ya kiingilio kwa ahadi ya faida kupitia usambazaji wa video.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Dar es Salaam, Faustine Mafwele, waliokamatwa ni pamoja na Hatibu Kudura, Fatum Hamisi na Athumani Sadik, kutoka maeneo kama Mbagala, Tabata, Ubungo na Mabibo. Uchunguzi wa polisi na BoT ulibaini kampuni hiyo haina uongozi maalumu.
"Vilevile ufanyaji kazi wake unahusisha kuwatoza wananchi kuanzia Sh50,000 na kuendelea ili uwe mwanachama, pia huchangisha fedha kwa kuwadanganya wananchi kuwa watapata faida kubwa kwa muda mfupi bila ya wanachama kuhusishwa kwa namna yoyote katika shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo," inaeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi wote kuacha kujihusisha na biashara za upatu mitandaoni bila kujiridhisha kwanza kwa kuwa baadhi ya biashara hizo hazina leseni wala vibali kutoka mamlaka za kisheria zinazohusika, hivyo kuhatarisha usalama pesa zao," inaeleza.
Source: Mwananchi