KERO Wafawidhi wa Vituo vya Afya hatuna posho ya madaraka kama ilivyo kwa wenzetu Wakuu wa Shule

KERO Wafawidhi wa Vituo vya Afya hatuna posho ya madaraka kama ilivyo kwa wenzetu Wakuu wa Shule

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa muda mrefu sasa hatupati posho ya madaraka, tofauti kabisa na wenzetu wa sekta ya elimu hasa wakuu wa shule za msingi ambao wao wanalipwa posho hiyo, hadi kufikia laki mbili kwa mwezi. Sisi Wafawidhi wa Vituo vya Afya, kuanzia ngazi ya hospitali hadi zahanati, hatupati chochote.

Ninazungumzia hali halisi iliyopo Mkoa wa Mara, hususan Wilaya ya Bunda, ambapo hakuna hata Mfawidhi mmoja anayepokea posho ya madaraka lakini kadri tunavyojua, hii siyo Bunda au Mara pekee inaonekana ni changamoto ya nchi nzima kwa Wakuu wa Vituo vya Afya.

Kilichokuwa kinatupa matumaini ni ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kwamba serikali ingeanza kulipa posho hiyo. Hata hivyo, hadi leo hakuna utekelezaji wowote. Sasa inaelekea miaka miwili inapita tangu ahadi ile itolewe bila hatua yoyote kuchukuliwa.

Soma Pia: Mshahara wa Waganga wafawidhi wa Zahanati na vituo vya Afya hauna tofauti na wa Daktari wa kawaida, Serikali itupatie posho ya madaraka

Hali hii inakatisha tamaa, kwani tunabeba majukumu makubwa ya kusimamia vituo vya afya, lakini hatutambuliwi kwa stahiki zetu kama ilivyo kwa sekta nyingine.

Tunaomba serikali itazame upya suala hili na kutekeleza ahadi iliyotolewa, ili nasi tupate haki yetu kama watumishi wengine wa umma.
 
Poleni.Tamko lilitoka muongozo hakutoka? au muongozo ulitoka viongozi wakaupuuza?.Wizara husika naamini watalifanyia kazi.
 
Hadi nimecheka, vikao vya mara Kwa mara ndio posho zenu, call, overtime mnazopata kuliko wengine hizo ndio posho zenu mganga mfawodhi,

Na pesa za basket fund zinazo kuja mnajikatia juu Kwa juu,

Kuna pesa za bima ya afya
 
Vilio kuhusu njaa na magego kuuma ni kila pembe ya hili getho kubwa Afrika Mashariki.
 
Back
Top Bottom