Hawa ni baadhi TU ya waandishi wa habari wa bongo walio fanyiwa vitendo vya kihuni na vyombo vya usalama. List ni ndefu na tukisimulia tunakumbushia machungu🥺
Azory Gwanda - Mwandishi wa habari aliyejulikana kwa kuchunguza matukio ya uhalifu huko Rufiji, alitoweka mnamo Novemba 2017 na hadi leo hajulikani alipo. Azory alikuwa akiandika kuhusu mauaji ya viongozi wa vijiji na polisi katika eneo hilo.
View attachment 3093259
Maxence Melo - Mwanzilishi wa JamiiForums, aliwahi kushikiliwa na vyombo vya usalama kutokana na msimamo wake wa kutokutoa taarifa za watumiaji wa tovuti yake. Maxence amekuwa akikumbana na shinikizo kwa kazi yake ya kuchapisha habari za uchunguzi.
View attachment 3093261
Erick Kabendera - Mwandishi huyu alikamatwa mnamo Julai 2019 na kushitakiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha, ukwepaji kodi, na uongozi wa genge la uhalifu. Kabendera alikuwa akiandika kwa vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu masuala ya kisiasa nchini Tanzania.
View attachment 3093257
Salma Said - Mwandishi kutoka Zanzibar aliyewahi kushambuliwa na kikundi cha watu wasiojulikana mwaka 2015. Tukio hili liliripotiwa kuhusishwa na kazi yake ya uandishi wa habari, hasa wakati wa uchaguzi wa Zanzibar.
View attachment 3093256
List Bado ni ndefu ....