Wafu kufufuliwa au kutofufuliwa kulingana na maandiko

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
142
Reaction score
281
Wafu kufufuliwa au kutofufuliwa kulingana na maandiko

Katika kitabu cha Ayubu 14:12 tunasoma kuwa wafu hawafufuliwi. Katika kitabu cha 1Wakorintho 15:51 tunaona biblia inasema wafu watafufuliwa. Je, biblia imejichanganya?

Tuelewe kabisa kuwa biblia kamwe haijichanganyi, wala haijawahi kujichanganya. Tafakari zetu ndizo zinachojichanganya. Maeneo mbalimbali kwenye biblia, yanakamilishana, wala hayajichanganyi. Biblia lazima isomwe yote na siyo kusoma sehemu chache tu na kuishia njiani. Ukisoma biblia yote, utagundua kuwa haijichanganyi.

Turejee mistari hiyo na kisha tuone majibu yake kupitia biblia hiyo hiyo.

Ayubu 14:10 “Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? 11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; 12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.”

Ni kweli hapa maandiko yanasema kuwa mwanadamu hulala chini, asiinuke tena.

Lakini, hebu turejee agano jipya katika kitabu kile cha Wakorintho, tuangalie biblia inatuambiaje:
1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Hapa, maandiko yanatuambia, parapanda italia na wafu waliolala katika Kristo watafufuliwa.

Swali: tuchukue lipi na tuache lipi?
Maneno kama hayo hayo, yanarudiwa tena katika 1Wathesalonike 4:16:
16 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza".

Jibu ni kuwa wafu watafufuliwa siku ya mwisho, sawa sawa na Yohana 5:25:
25 "Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai".
Je, ni kwa nini maandiko ya 1Wakorintho 15:51 yana nguvu kuliko yale ya Ayubu 14:12, yanayosema kuwa “wafu hawafufuliwi”? Hii ni kwa sababu Agano Jipya ni ukamilifu wa Agano la Kale.

Manabii waliotangulia walifahamu mambo kwa sehemu, lakini Roho Mtakatifu katika Agano Jipya, amekamilisha yote na kufunua yote.
Na kawaida ni kwamba unapokuja ule ufunuo mkamilifu, bali ule uliokuwa unajilikana kwa sehemu, unabatilika. Ndivyo maandiko yasemavyo:
1Wakorintho 13:9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”.

Manabii wengi wa Agano la Kale
hawakujua mengi kuhusiana na ufufuo, au mbingu mpya na nchi mpya, ingawa walikuwa wanafahamu siku moja watajua mambo yote, hivyo walitoa unabii kwa sehemu waliyopimiwa. Lakini mwisho wa nyakati, Roho Mtakatifu anakamilisha ufunuo wote sawa sawa na 1Wakorintho 13:9-10.

Kwa hiyo, kwa hitimisho, ni kwamba wafu watafufuliwa siku ya mwisho, na watahukumiwa:
Yohana 5:28 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.

Ikumbukwe kuwa hoja hii ya kufufuliwa kwa wafu ndiyo iliyoleta mgawanyiko mkubwa katikati ya Wayahudi, hata kuzaliwa makundi (madhehebu) mawili ambayo ni Mafarisayo na Masadukayo, ambapo Mafarisayo waliamini ufufuo na Masadukayo hawakuamini ufufuo, kwa kutumia andiko hilo la Ayubu 14:12 pamoja na maandiko mengine.

Lakini, Bwana Yesu alikuja kuondoa utata huo kama tunavyosoma kwenye Agano Jipya, katika Mathayo 22:23-32:
23 “Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai”.

HITIMISHO KUHUSU KITABU CHA AYUBU NA KITABU CHA 1WAKORINTHO

Hitimisho kuhusu kitabu cha Ayubu 14:12 na kitabu cha 1Wakorintho 15:51, ni kuwa wafu watafufuliwa. Hakuna mahali ambapo biblia inajichanganya, kwani katika biblia hiyo hiyo moja, kitabu cha Mathayo 22:23-32 kimekamilisha habari hiyo. Biblia ni lazima isomwe yote na siyo sehemu chache tu. Agano la Kale na Agano Jipya, maagano hayo yanakamilishana.

JE, SISI TUTAKUWA UPANDE UPI WAKATI HUO?
Baadhi ya watu hujiuliza, je, sisi tutakuwa upande upi wakati huo wa ufufuo? Je tutafufuliwa ili tukavikwe taji na kuurithi uzima wa milele, au kwa ajili ya hukumu ya ziwa la moto?

Kumbuka kuwa wote walio nje ya Kristo, ambao hawajampokea Bwana Yesu na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake, wametabiriwa kuwa miongoni mwa watakaohukumiwa katika hukumu ya milele. Je umeokoka? Umebatizwa katika ubatizo sahihi wa maji meni?
Je umejazwa Roho Mtakatifu?
Ni suala la uamuzi binafsi. Hata hivyo, ni heri kufanya uamuzi mapema wa kubadili njia ya maisha yako.
 
...Mimi nawabatiza kwa Maji Kwa ajili ya TOBA.
 
Uwo mwisho haujafika bado, ilakunawatu mnajifanya clips za mwisho wa dunia mnazo.

Djni ni biashara na career kama career nyengine
Unatumia sana akili zako kufikiria, punguza ujuaji na usome maandiko!
 
Iyo ni career yao bila kuwaambia hivyo awawezi pata kula. Akili kumkichwa.
Kula nini?? Wote wanaojifunza au wanaohubiri neno hawali mpaka wakuletee wewe neno ndio wanakula? Hiyo akili unayoizungumzia hapa sio ya kawaida!
 
Msingi wa Imani ya kikristo unajengwa na Biblia. Biblia imebeba Agano baina ya Mungu na wateule wake, japokiwa Biblia imeandikwa na watu wengi tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti jambo Moja tunapaswa kufahamu Biblia haifungamani.

Biblia imebeba Siri nzito ndio maana imeandikwa kwa mafumbo na mithali ukisoma math 13:34-35 tunaona yesu alitumia mifano na mafumbo katika mafundisho yake Yesu hakufanya hivi kwa bahati mbaya Bali alikuwa akitimiza unabii soma Zaburi 78:2. Lakini pia math 13:10-12 tunaona Kuna waliojaaliwa kuzijua Siri za ufalme wa mbinguni (wanafunzi ambao walimpokea yesu)
Ukielewa maana ya mafumbo na mifano iliyopo katika Biblia kupitia Biblia yenyewe (mithali 30:5-6) unaweza kutambua kilichozingumzwa katika Biblia, mfano ukisoma
Mathayo 13:31-32
[31]Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;
[32]nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake. Kuelewa ufalme wa Mungu kupitia mfano huu, kwanza kupitia Biblia tunatakiwa kujua maana ya vitu vifuatavyo, 01. Mbegu, 02. Shamba, 03. Mti, 04. Matawi, 05. Nyuni (ndege). Shida huja pale tunapotafakari Maneno ya Mungu kwa kutumia mawazo ya wanadamu.

Ikumbukwe hakuna theolojia Duniani inayoweza kufafanusha Maneno ya Mungu isipokuwa Mungu mwenyewe kupitia neno lake. Hata ujio wa kwanza wa Yesu walikuwapo viongozi wakubwa wabobezi katika torati walikuwa wakisubiri ahadi ya Mungu kuletewa masihi mkombozi(Yesu). Ajabu alipokuja hawakuweza kumpokea na ikumbukwe Yesu alikuja kwa mujibu wa maandiko yaani torati yote ilikuwa ikimshuhudia Yesu ila viongozi wa dini (mafarisayo na masadukayo) walishindwa kutambua masihi wakamuua sababu walitumia mawazo Yao kufafanua Maneno ya Mungu.

Mungu ni Alfa na Omega, Ni Alfa kwasababu yeye hutoa ahadi (unabii) yaani mapango mzima jinsi itakavyokuwa, Na Omega ikimaanisha Mungu hutimiza ahadi yake kama alivyoahidi. Mfano ujio wa kwanza wa Yesu tunaona Kuna waliompokea akawapa haki ya kuwa wana wa Mungu, lakini pia Kuna waliomsulubisha pande zote mbili walitimiza unabii.

Mimi na wewe Leo tunasubiri kuja kwa Yesu mara ya pili maandiko yanasema atakuja na mawingu na kila jicho litamwona🤔 lakini pia maandiko pia yanasema atakuja kama mwizi usiku heri akeashaye. Kipi sahihi kati ya hivi viwili?. Tukumbuke Biblia imebeba Siri Kuna mambo makubwa na mazito yamefichwa kwenye maandiko, hakuna njia nyingine ya kimjua Mungu nje ya neno lake.

Ukisoma Yeremia 33:3 Mungu yupo tayari kutusikia na kuweka wazi Siri yake ikiwa tunamtafuta kwa dhati ya kutaka kimjua, neno lake linajitosheleza haliitaji nyiongeza ya tafakari za wanadamu. Ufunuo 22:18-19.
 
Nadhani ni kifo Cha kiroho kinazungumziwa zaidi ila sio kufufuliwa ukishakufa
 
Back
Top Bottom