Wafuasi wa Bobi wine wamiminika nje ya Hotel aliyofikia

Wafuasi wa Bobi wine wamiminika nje ya Hotel aliyofikia

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Kundi kubwa la wafuasi wa mgombea Urais wa Uganda kupitia chama cha National Unit Platform (NUP), Robert Kyagulanyi Ssentamu (Bobi Wine) wamemiminika nje ya hoteli aliyofikia katika mji wa Busia asubuhi ya leo huku mgombea huyo akijitokeza roshani mwa jengo hilo na kuwasalimu.

Kupitia chapisho aliloweka katika akaunti yake ya Instagram, Bobi Wine ameandika "huu ni muonekano kutoka kwenye baraza yangu eneo la Busia asubuhi ya leo. Inaonekana itakwenda kuwa siku nzuri"



Mwanasiasa huyo mkuu wa upinzani nchini humo anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini Uganda na leo atafanya kampeni katika mji huo wa Busia akinadi sera zake dhidi ya Rais aliye madarakani Yoweri Museveni ambaye anagombea Urais kupitia chama cha NRM.
 
Sikilizia hayo matokeo sasa uone mikeka inavyochanika.
 
Back
Top Bottom