ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Hayo ndio yanayojili huko Chadema baada ya Tundu Lisu kumkejeli Mwenyekiti wake Kwa kusema eti aliyetuaminisha kwenye mapendano yao amekamatwa,hii iwe fundisho 🤣🤣🤣.👇👇
Pia soma
LGE2024 - Lissu: Kukamatwa kwa Mbowe iwe fundisho tusirudie kudanganywa danganywa
Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe
LGE2024 - CHADEMA yatoa tamko baada ya Freeman Mbowe kukamatwa na Jeshi La Polisi
---
"Muda wa kuchekeana na CCM na uishe sasa, leo (jana) wamemkamata aliyekuwa akituaminisha kwamba watatuongoza kwenye mapendano hayo, wamemkamata, na hii iwe fundisho na tusije kurudia tena kudanganywa na kudanganyika."
Hiyo ni kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz) Bara, @TunduALissu, alipokuwa akilitaka Jeshi la Polisi kumwachia huru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, bila masharti.
Lissu ametoa kauli hiyo Novemba 22, 2024, wakati akiwanadi wagombea wa Serikali za Mitaa katika wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Kauli ya Lissu imeibua mjadala mkali ndani ya chama hiko, ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA wameonesha kutokubaliana naye.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, Jackson Malisa, akizungumza na Jambo TV mapema leo Novemba 23, 2024, amesisitiza kuwa maamuzi ya chama hiko kukubali maridhiano hayakufanywa na mtu mmoja bali yalipitishwa na kamati kuu ya chama kwa nia njema ya kulijenga taifa.
“Dhamira ya Kamati Kuu ya CHADEMA kukubali maridhiano ilikuwa ni ya kutaka kuliunganisha taifa. Matokeo yoyote ya maridhiano, iwe yamekidhi matarajio au hayajakidhi, si vyema matokeo haya akabebeshwa mtu mmoja, kwani maamuzi hayakufanywa na mtu mmoja bali Kamati Kuu nzima kwa niaba ya chama,” alisema Malisa.
Malisa ameendelea kusisitiza kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, asibebeshwe lawama zozote kwa matokeo ya maridhiano hayo, kwa kuwa azimio la maridhiano lilifanywa kwa pamoja na Kamati Kuu, na Mwenyekiti alitoa tamko hilo kwa niaba ya chama.
Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Tundu Lissu imeibua hisia mseto na kuonesha uwepo wa tofauti za kimtazamo miongoni mwa viongozi wa chama kuhusu suala la maridhiano na namna ya kushughulikia changamoto zinazotokana na siasa za vyama vingi nchini.
Hata hivyo, baada ya kushikiliwa kwa saa 12 na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), @freemanmbowetz na wenzake 10 wameachiwa huru.
Mbali ya Mbowe, wengine ni Joseph Mbilinyi @TheRealJongwe 'Sugu' (mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Pascal haonga(mbunge wa zamani wa Vwawa), Apporinaly Boniface (Mkuu wa Kitengo cha Digital- CHADEMA), Paul Joseph naCalvin Ndabila (maofisa Habari wa Kanda ya Nyasa).
Pia wamo, Khalfan Mbwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wanya (walinzi wa Mbowe), mwenyekiti wa ACT-Wazalendo mkoa wa Songwe, Ezikia Zambi.
Wote hao walikamatwa na jana Ijumaa Novemba 22, saa saba katika mchana katika Pori la Halungu wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, Augustino Senga, Mbowe na wenzake, walishikiliwa kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kampeni, wakitaka kufanya mkutano eneo ambalo hawakupangiwa.
Chanzo: Jambo Tv
My Take
Chama ambacho Kila mtu ni kambale hakina tofauti na kikoba .