Wafuasi wa viongozi wa dini wanishukia kama mwewe

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
WAFUASI WA VIONGOZI WA DINI WANISHUKIA KAMA MWEWE​

Na, Robert Heriel

Juzi niliandika makala inayomzungimzia kiongozi wa kidini aitwaye Gwajima. Nikizungumzia baadhi ya kauli zake mbaya ambazo kimsingi ndizo zinanifanya nimuandame, yeye na watu wenye tabia kama zake.

Sikuandika kwa sababu ninamchukia Gwajima, au ninaagenda ya siri ya kutaka Gwajima asiwe Mbunge, bali niliandika nikiwa nimedhamiria kuwa Watu mfano wa Gwajima wanapaswa wakemewe kwa makemeo yaliyodhahiri. Moja ya mambo ambayo siyapendi ni kuona ubaguzi, udini, ukabila hasa ukifanywa na watu wenye nafasi.

Niseme tuu, Taikon hana maslahi na chama chochote, hana maslahi na mtu yeyote. Na hataki maslahi ya mtu yeyote wala chama chochote. Taikon nina maslahi na nchi hii kwa sababu, ndipo ninapoishi, ardhi yake inanipa chakule, nchi hii ndio nitapata mke na watoto, nchi hii ndio nitakayozikwa, watoto wangu wataishi humu. Hivyo ni lazima nihakikishe nchi hii inabaki salama hata kwa nafasi ndogo niliyonayo.

Wafuasi wa viongozi wa dini walinipigia wakinilaani, wakinikemea, wakinitusi, wakinitolea maneno ya kila namna waliyoona yanaweza kunidhuru kisa nimemsema kiongozi wao, na watu wenye tabia kama yake.

Moja ya maswali waliyoniuliza ni haya;

1. KWA NINI UNAWASEMA VIBAYA VIONGOZI WA DINI? HUJASOMA KUWA HUPASWI KUWATUSI WATUMISHI WA MUNGU?
Majibu;

Sijawasema vibaya viongozi wa dini, ila nimewaambia ukweli na kukemea mahali walipoteleza.
Kisha nikawauliza Mtumishi wa Mungu ni nani?
Akanijibu, ni mtu anayeshughulika na mambo ya Mungu.
Nikauliza, Mambo ya Mungu ni yapi, nitajie matatu?
Akajibu, kuhubiri injili na habari zake.
Nikamwambia, Jambo la pili na la tatu?
Akakaa kimya. Nimamwabia kwa hiyo Mungu anajambo moja tuu?

Nikamuuliza, unakijua kitabu cha Daniel? hakujibu, akaniambia niendelee. Nikamuuliza unamjua Mfalme Nebukadreza?
Je, yeye alikuwa anahubiri habari za Mungu?

Nikamwambia; Kila mtu unayemuona hapa duniani ni mtumishi wa Mungu, sema kila mmoja anaidara yake. Wengine wanamtumikia Mungu kuwashonea watu viatu, kuendesha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kulimia watu chakula, kuongoza watu, kufundisha, kutibu watu, kusimamia sheria, kulinda wananchi na mali zao. Hao wote wanamtumikia Mungu kupitia kazi walizopewa na Mungu.

Mtu yeyote anayefanya kazi kuhudumia watu kwa njia iliyohalali na kufuata sheria za Mungu na nchi mtu huyo ni Mtumishi wa Mungu.

Yeye akaniambia ati tunapaswa tuwaheshimu viongozi wa dini na watumishi wa Mungu(akimaanisha wachungaji, askofu, masheikh n.k) zaidi kuliko watu wengine.

Nikamwambia watu wote wanapaswa kuheshimiwa kwa sababu wote ni watumishi wa Mungu. Kila mtu anastahili heshima ikiwa tuu anafanya iliyohaki mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

Binadamu yeyote bila kujali yupoje anakemewa ikiwa atavunja sheria za Mungu au za nchi. Hakuna aliyezaidi ya mwingine. Ati Daktari akikosea asikemewe kisa ni Daktari, lakini mpiga debe akemewe kisa ni mpiga debe yaani kazi yake haina maslahi.

Nikaendelea kusema; Mtu yeyote ikiwa anataka asikemewe basi afanye haki ya Mungu tena ashike sheria za nchi, na ikiwa sheria zitaingilia haki ya Mungu basi azipinge kwa nguvu zote.

2. UNAMKANYA GWAJIMA KWA MAMLAKA IPI, NANI KAKUPA MAMLAKA YA KUMKANYA MTUMISHI WA MUNGU?
Hakuna aliye na Mamlaka zaidi ya mwingine katika kukemea uovu. Mtu yeyote anaowajibu wa kukemea maovu. Hakuna aliyepewa haki miliki ya kukemea uovu. Uovu unakemewa na mtu yeyote anayejielewa, anayemheshimu Mungu, anayependa amani, anayependa haki.

Siku hizi maovu yameongezeka kwa sababu waovu wanajiundia sheria batili zitakazo wabana. Mfano, zamani mtoto anapokosea labda mtaa wa pili, mtu yeyote anaweza akamuadhibu na wala pasiwe na shida. Lakini zama za sasa waovu wameunda mfumo ambao hautakupa nafasi kuupinga uovu wafanyao watoto. Ukimpiga mtoto wa mtu usishangae ikawa kesi kubwa, au mtoto akakuambia kwani wewe ni Baba yangu, au Mama yangu. Hii ni dalili ya kuwa zama hizi tunaishi katika jamii iliyoharibiwa na uovu.

Mtu yeyote anaowajibu wa kukemea uovu bila kujali ni nani kaufanya, kumbuka watu wote ni sawa mbele za Mungu, hivyo hata akikosea Daktari, Mwalimu, Mchungaji, Sheikh, imamu, n.k

Kumbuka Uchungaji, uaskofu, usheikh, uimamu zote ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

3. HUOGOPI LAANA YA MUNGU KWA KUWASEMA WATUMISHI WA MUNGU?
Siogopi. Ikiwa nitawasema pale wanapokosea na kukengeuka, nitawasema. Nitawakosoa vilivyo kila nipatapo nafasi na kila ninaposikia wanafanya uovu.

Sio watumishi tuu hata watu wa kawaida, viongozi wa kisiasa n.k. Siogopi kuukemea uovu.

Hakuna Mungu Duniani na Mbinguni wa Kunipa laana pale ninapokemea uovu, uonevu, ninapotetea haki.

Naogopa laana ya Mungu, pale nitakapoona Mtumishi wa Mungu anakemea uasi alafu mimi namtukana, naogopa laana ya Mungu pale ninapoona mtumishi wa Mungu anahamasisha upendo ndani ya Jamii alafu mimi nimseme vibaya. Lakini sio kiongozi aendekeze utengano kwa kuhamasisha udini, ukabila au namna yoyote ya kuvuruga jamii.

4. HUONI UNAPOMSEMA KIONGOZI WA DINI UNAAMSHA HISIA ZA WAFUASI WAKE?
Kupitia kumnyoosha kiongozi wa dini hata wafuasi wake watakuwa wamenyooka, lakini kumuacha aendekeza mambo yasiyofaa ni kuruhusu na wafuasi wake wafanye kama kiongozi wao anavyofanya.

5. UNAJIAMINI NINI MPAKA UMSEME MTU MKUBWA KAMA GWAJIMA?
Naamini katika haki ya Mungu na kufuata sheria za nchi, sijiamini kama nitaona uovu unafanyika, nikausikia au kuuona alafu nikaunyamazia. Hapo kujiamini kwangu kunapungua kwa maana najua ikiwa uovu huo amefanyiwa mwingine basi hata mimi ipo siku nitafanyiwa. Najiamini kukema uovu maana kupitia hivyo muovu akiacha tabia yake basi hata mimi nitakuwa salama. Lakini siwezi kuwa salama kwa kuacha uovu uendelee kisa haunihusu, najua kadiri uovu ninavyouachia uendelee ndivyo ninapoupa nafasi unikaribia na utanikaribia na kuniangamiza.

6. HUOGOPI KUPOTEZWA KWA KUKEMEA VIONGOZI?
Siogopi. Naogopa kukaa kimya na kuunyamazia uovu. Kama Mungu amenipa nafasi ya kuukemea acha niukemee. Na kama Mungu aliyenipa nafasi ya kukemea uovu akawapa nafasi ninaowakemea wanipoteze kwangu haitakuwa shida, kwani misheni itakuwa imekamilika.

7. KWANI TAIKON WEWE NI CHAMA GANI?
Mimi sina chama, sina dini, sina timu. Nipo huru. Nikitaka burudani ya mpira naangalia mpira na nafurahia yeyote atakayeshinda, silazimishi timu fulani ishinde, atakayecheza vizuri na kutumia udhaifu wa mpinzani wake akishinda kwangu ni furaha. Nasikilizi sera za vyama vyote, namsikiliza Mhe. Rais Magufuli wa CCM, namsikiliza Tundu Lisu wa CHADEMA, Mhe Membe wa ACT n.k. Nasikiliza hoja, ukizingua kwenye hoja nasema umezingua, ukisema vyema nakupongeza, nipo huru na nafurahia maisha.

Naingia kusikiliza mafundisho ya dini zote, nikiwasikia waislam wanatoa mawaidha yanayofaa nawapongeza, wakristo nao nawapongeza, wabudha nao nawapongeza, wapagani nao nawapongeza, ilimradi mafundisho yasiyodhuru mtu, yasiyoumiza mtu, yasiyoharibu utu, asili, na mazingira. Nafurahia maisha. Nasoma vitabu vyote, sina mipaka katika kujifunza ikiwa mafunzo hayo hayana dalili ya uasi kwa Mungu au uvunjifu wa sheria za nchi. Nipo huru.

Mwisho wafuasi wa dini walinisihi niache kumsema kiongozi wa dini. Nami nikawajibu, nitaacha ikiwa sitaona kauli itakayoathiri maslahi ya jamii ambapo mimi ninaishi.

Kilichonishangaza, nilipomuuliza swali mfuasi Mmoja kuwa; Kati ya Mungu na watumishi wa Mungu unampenda nani na unamsikiliza nani? Walichonijibu, nilicheka sana, pia nilitambua kuwa ninaongea na watu wa namna gani. Walinijibu; wanawapenda wote, Mungu na watumishi na Mungu. Nikawauliza nani anatangulia, je Mungu au watumishi wake, wakajibu hakuna. Nilicheka sana.

Mimi sina shida na mtu, ni kijana ninayekubali maonyo, na kijana ninayetoa maonyo ikiwa mtu amekengeuka. Sipendi nizungukwe na watu wanaoshindwa kunionya ati kwa kunionea aibu, kwa maana mimi sina unafiki. Nyeusi ni nyeusi na kijani ni kijani.

Mwisho niseme; Watu wote tupo kwa ajili ya Mungu, tunaishi kwa Mungu na tutaondoka kwa Mungu. Tupendane lakini kama miongoni mwetu hata ikiwa ni mimi ni/atakengeuka basi sharti nikemewe kwa nguvu zote.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kutoka Nyota ya Tibeli
0693322300
 
Hongera sana mkuu inaonekana unauelewa mpana na mambo ya MUNGU, Gwajima siyo mtumishi wa MUNGU ni mchuuzi/machinga wa dini kama walivyo machinga wengine, hakuna mtu mwenye akili timamu utamkuta kwenye mabanda ya watumishi kama akina Gwajima, ukikuta mtu humo ujue amekata tamaa na maisha anaishi kwa faraja, waumini wao huwa ni maskini wa kutupwa lakini viongozi wao ni matajiri haswa, wanaambiwa mtolee MUNGU chochote ulichonacho kwa ahadi kuwa wataongezewa matokeo yake wana baki kuwa maskini wa kutupwa. Mkuu achana na hayo matapeli.
 
Umenena vema. IGP kalizungumzia hilo. Kasema mhalifu ni mhalifu tu, hata akiwa Padri, Askofu, Mchungaji au Shehe atachukuliwa kama mhalifu na sheria itafuata mkondo wake bila kuogopa title yake.
 
Duh. Una moyo mkubwa. Kubishana na mashabiki wa mtu.
 
Back
Top Bottom