Wafuatao wajiandae kumrithi Rais Dkt. Magufuli mwaka 2025 tafadhali

Wafuatao wajiandae kumrithi Rais Dkt. Magufuli mwaka 2025 tafadhali

Acha ubabaishaji wewe! Kama kweli tupo serious na tunapenda maendeleo ya nchi yetu Tanzania basi mimi naona baada ya Magufuli rais ajae wa Tanzania yetu ni Mheshimiwa TUNDU ANTIPAS LISSU. Ni mzalendo, muwazi, jasiri, mwenye maono n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ummy Mwalimu ni MTanga siyo Mzanzibar, katiba inasema makamu wa rais shart atoke Zanzibar

Niwekee hapa hiyo Katiba ya CCM au ya nchi ambayo ina sehemu inayosema kuwa ni lazima kuwe na mabadilishano ya Uongozi kati ya Wazanzibara na Wazanzibari. Watanzania hebu acheni Kukariri jamani. Hivi mwaka 2005 Rais Mstaafu wa awamu wa Tatu Mzee Mkapa alipotoka Madarakani aliyemuachia Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mzee Kikwete alikuwa ni Mzanzibari?
 
Wakati unawaandika ulikuwa umefumba macho na brain!!! Maana wengine hapo kuwataja inahitaji moyo labda unaundugu nao na huwatakii mema watanzania.
 
Mtabiri hahaha,nakuona mzee wa kushindilia maandishi.
Hii nayo umepenyezewa kutoka katika vyombo vyako?
 
Watanzania kwa asilimia 100% hakuna aliye mtabiri JPM kukamata madaraka haya makubwa aliyo nayo....!!

Wengi tulimfikiria Lowassa na baadae B. Membe....

Hivyo kama ni Utabiri, ama ni ndoto umelala ukaota hivyo, ni bora mleta mada ukaendelea kulala tu, ili kuimarisha na pengine kufanya ndoto yako kuwa ya kweli...!!

Kila la kheri kwa wote ulio wataja kuongoza/kutuongoza kesho...

Sent using Jamii Forums mobile app
Pasco wa humu JF alitabìri khs Magu.
 
Acha ubabaishaji wewe! Kama kweli tupo serious na tunapenda maendeleo ya nchi yetu Tanzania basi mimi naona baada ya Magufuli rais ajae wa Tanzania yetu ni Mheshimiwa TUNDU ANTIPAS LISSU. Ni mzalendo, muwazi, jasiri, mwenye maono n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usishangae, hizi ndizo akili zetu za kitanzania hata tukiwekewa pazia tutalichagua kama litakuwa na green/yellow color!
 
okay unamaanisha uchaguzi wa 2020 umeshafanyika na magu ameshinda
 
Nimeweka Kitu cha Kiutafiti, Kiuchambuzi na cha Kimkakati hasa wa Ushindi kwa CCM huo mwaka 2025. Hao wakiteuliwa na Chama kama nilivyoainisha hapo halafu wakajipanga kama nilivyopanga basi Tanzania itaendelea kufurahia Uongozi mzuri wa Chama Tawala ( Chama changu pia ) cha CCM kwani nawaamini 100% hao Watajwa na nawakubali mno. Ukiona hadi GENTAMYCINE anakukubali jua hata Mwenyezi Mungu ameshakuwekea tiki na amekukubali kwani Mimi ni Malaika wake wa Kutukuka kabisa hapa duniani.
Umemwacha January Makamba na Mwigulu Mchemba uzi wako umepoteza mantiki!
 
Wakijilinda Kiafya na kuzidisha sana maombi yao ya Utendaji huku wakiwa waaminifu na wenye moyo hasa wa Kiuzalendo na Mapenzi ya dhati kabisa kwa nchi ya Tanzania basi wafuatao watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Dkt. Hussein Mwinyi
Makamu wa Rais Jennister Mhagama
Waziri Mkuu Suleiman Jaffo

Endapo hao Watajwa hapo juu Mwenyezi Mungu hatotubariki kuwa nao hadi huo mwaka wa 2025 basi wafuatao wajiandae kuchukua nafasi zao endapo tu na Wao watalinda afya zao, kuzidisha maombi yao kwa Mwenyezi Mungu, wakiwa waaminifu hasa bila kusahau wawe Wazalendo wa kweli kwa nchi ya Tanzania basi watakuwa Warithi sahihi na wazuri sana wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimaliza muhula wake wa pili hapo mwaka 2025

Rais Professor Makame Mbarawa
[Makamu wa Rais Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu Luhanga Mpina

Ombi kwa Watajwa hao hapo juu tafadhalini......

  • Tunzeni afya zenu ( HILI NAOMBA MLIZANGITIE SANA )
  • Jiheshimuni sana ( maisha ya Kihuni / Kisela / Kisanii sasa kaeni nayo mbali )
  • Zidisheni uadilifu wenu
Ombi langu Kuntu kabisa kwa Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli juu ya hawa Watajwa ni kwamba.....
  • Waamini sana hao niliowataja hapo juu
  • Wazidishie Ulinzi wao kwani ndiyo Warithi wako wazuri na watarajiwa
  • Wajenge zaidi hasa Kiitifaki
Kila la kheri na ni matumaini yangu makubwa Kwako Mheshimiwa Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Magufuli kuwa Mimi GENTAMYCINE nimekurahishia Kazi yako ya kuwakabidhi nchi akina nani hapo mwaka 2025 utakapong'atuka na hao ndiyo pekee watakaokufaa kwani wana uthubutu wa kupita mule mule ambako umepita Wewe na kuzidi kuiletea Maendeleo hii nchi yetu.

Nawasilisha.

Hapo kwenye red umeongelea rais au au makamu wa rais?
 
Mtoa mada 2015 ulisemaga Raisi atakua PROF. MUHONGO mpk leo tumeachiwa manyoya tu

Siko huko tena nimeshatoka sasa ni mwaka 2017 na nakuomba hapo hapo katika huo huo uzi uliousoma na kusema hivyo ulivyosema Wewe angalia tena uzi mwingine wa nini nilichokisema kuhusu Rais Dkt. Magufuli halafu niambie je kilitokea au hakijatokea? Tatizo lenu mnang'ang'ania huo uzi niliomtaja Waziri Professor Muhongo halafu ule uzi niliopatia wa kumhusu Rais Dr. Magufuli hamuutaji.

Endeleeni kupiga majungu yenu ila tambueni tu kwamba GENTAMYCINE ni ' Purely Talented and Charismatic Fella '. Kazi Kwako / Kwenu.
 
Mkuu Ummy Mwalimu ni MTanga siyo Mzanzibar, katiba inasema makamu wa rais shart atoke Zanzibar
Wrong!!

Katiba inataka iwapo Rais atatoka bara basi makamu atoke Visiwani and vice versa ............. Sasa Mbawara ni ZNZ wakati Ummy ni Bara. Hakuna tatizo hapo!! Ila Gentamycine anatulisha changa .....!!
 
Acha ubabaishaji wewe! Kama kweli tupo serious na tunapenda maendeleo ya nchi yetu Tanzania basi mimi naona baada ya Magufuli rais ajae wa Tanzania yetu ni Mheshimiwa TUNDU ANTIPAS LISSU. Ni mzalendo, muwazi, jasiri, mwenye maono n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unamuongelea huyu LISSU aliyesimama kuwatetea wazungu au mwingine!!
 
Kana akili za kitoto mno

Nyota Kali ya ' Purely Talented and Charismatic Fella ' inakutesa sana Mkuu. Pole sana na kadri unavyozidi kuniandama ukidhani labda unanimaliza au unanipunguza Kasi yangu humu JF ambayo inakuumiza basi ndiyo Kwanza unazidi kunifanya nifuatiliwe, nipendwe na nikubalike na wengi.

Badala ya Kunichukia au kunionea Kijicho ungetumia tu muda wako uniulize ni kwanini nakubalika na naweza kuja na Threads ambazo zinawavuta Watu wengi hadi GENTAMYCINE sibanduki akilini na mioyoni mwao ili angalau na Wewe uoshe nyota.

Mwisho nikusihi tu Mkuu usiache Kunichukia au Kunifuatafuata humu JF kwani ni nyie mnaonichukia humu JF ndiyo mnanifanya kila siku nizidi tu kutafuta mbinu mpya za kuwazidi Kimaarifa na Kimkakati hadi mnaona leo nipo hivi huku nanyi mkiwa hivyo.
 
Umemwacha January Makamba na Mwigulu Mchemba uzi wako umepoteza mantiki!

Nisamehe na nikuombe sana radhi kwa kuwaacha hao wanaokuweka Mjini Mkuu. Usijali nitawaja siku si nyingi pale ambapo Baraza la Mawaziri litakapoenda kubadilishwa ambapo kuna uwezekano hao Wanaokuweka mjini wasiwepo tena ( nikimaanisha ) watabadilishwa. Stay tuned!
 
Back
Top Bottom