Wafugaji: Tupeane elimu ya Azolla ili tupunguze gharama za chakula kwa mifugo

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Posts
10,518
Reaction score
13,144
Mimi ni mfugaji katika kutafuta njia za kupunguza gharama za chakula cha mifugo ndipo nilipokutana na maelezo kuhusu Azolla kwamba imewasaidia wafugaji wengi kupunguza gharama za chakula cha mifugo kwa asilimia kubwa

Nikaona nije kujadiliana na wafugaji wenzangu hapa ili tuweze kupatiana elimu juu ya mambo yafuatayo kuhusu Azolla.

1. Upatikanaji wa mbegu
2. Jinsi ya kuweza kuotesha
3. Ulishaji wake kwa mifugo

Na mambo mengine muhimu juu ya hii Azolla
Hizi ni baadhi ya picha nilizipata kwa wafugaji wengine wanaotumia Azolla kulisha mifugo

Mkuu hii azolla au ina jina jingine? Maana nimetafuta mbegu zake karibu mwezi mzima bila mafanikio. Nipo dar es salaam.
 
Asante mkuu,ngoja tuendelee kuisaka ilimu juu ya hii Azolla kwani inaonekana mkombozi kwetu sisis
 
Mkuu hii azolla au ina jina jingine? Maana nimetafuta mbegu zake karibu mwezi mzima bila mafanikio. Nipo dar es salaam.

Tukipata taarif sahihi tushtuane

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Mkuu jina ni hilo hilo na muonekano ni huo huo kama unavyoonekana kwenye picha,kwa kua uko dar hebu jaribu kumcheck huyu ndugu niliona ameweka tangazo anauza mbegu,ukifanikiwa fanya kuja kutupa mrejesho[emoji116]
 
Ngoja nimcheki nitawapa mrejesho.
 
Mkuu hii azolla au ina jina jingine? Maana nimetafuta mbegu zake karibu mwezi mzima bila mafanikio. Nipo dar es salaam.
Nenda baharini mkuuu ukingo vwa bahari utaona kijito cha maji Azola zimeota pembeni mimi mbegu nilichukua ufukwe wa rainbow (mbezi beach) madukani nilizunguka sana kutafuta.
 
Wakuu mrejesho ni kwamba nilifanikiwa kuwasiliana na yule mtu japo bei yake anasema anauza kilo moja kwa shilingi elfu thelathini. Sasa hapo nikaona kama hatutakuwa tumeepuka gharama.
 
Nenda baharini mkuuu ukingo vwa bahari utaona kijito cha maji Azola zimeota pembeni mimi mbegu nilichukua ufukwe wa rainbow (mbezi beach) madukani nilizunguka sana kutafuta.
Nashukuru kwa ushauri huu. Nitaufanyia kazi. Pia inaonekana una uzoefu na hii kitu. Unaweza tusaidia hatua za kufanya. Kuanzia upandaji wake, matunzo pamoja na wastani wa kiasi kinacho weza kupatikana. Nashukuru
 
Kuna Huyu jamaa Yupo mlandizi kibaha anaweza kukupa Elimu nzuri tu na mbegu za Azolla
Namba yake 0659 134505
 
Azola inafaa hata kwa mifugo ng'ombe,na je ukizalisha azola kibiashara ukauza kwa wenye mahitaji inalipa??
 
Azola inafaa hata kwa mifugo ng'ombe,na je ukizalisha azola kibiashara ukauza kwa wenye mahitaji inalipa??
ndio inafaa na ata kuilima kibiashara ina faida na haina process kwa kua inajizalia kama magugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…