Wafugaji: Tupeane elimu ya Azolla ili tupunguze gharama za chakula kwa mifugo

Wafugaji: Tupeane elimu ya Azolla ili tupunguze gharama za chakula kwa mifugo

Mimi ni mfugaji katika kutafuta njia za kupunguza gharama za chakula cha mifugo ndipo nilipokutana na maelezo kuhusu Azolla kwamba imewasaidia wafugaji wengi kupunguza gharama za chakula cha mifugo kwa asilimia kubwa nami nikaona nije kujadiliana na wafugaji wenzangu hapa ili tuweze kupatiana elimu juu ya mambo yafuatayo kuhusu Azolla.
1.upatikanaji wa mbegu
2.jinsi ya kuweza kuotesha
3.ulishaji wake kwa mifugo
Na mambo mengine muhimu juu ya hii Azolla
Hizi ni baadhi ya picha nilizipata kwa wafugaji wengine wanaotumia Azolla kulisha mifugo
106913b695048788b7a7dd30f43852f4.jpg
7cbf8a2fa2a4cb3d2df00a9df5f153e0.jpg
2553103bf0ebf212f7895670ce9785e0.jpg
f14144826f60d950128956b5ff324dc7.jpg
5bca511fc82c5bf92d3a619bd4038f33.jpg
908a9de9249e74e4be8de7332612c96a.jpg
0897199ef287c2c297b328a9de6a0cae.jpg
Yeah hii azolla ni nzuri sana na inapunguza gharama za chakula kwa asilimia kubwa sana, na utengenezaji wake ni rahisi kwa garama ndogo
 
Kwa ambao mko bagamoyo na maeneo jirani.....Ninayo azola ya kutosha kwa ajili ya mifugo yangu pia ninatoa maelekezo kuhusu azola na mbegu pia! 0654255175
 
Mkuu hii azolla au ina jina jingine? Maana nimetafuta mbegu zake karibu mwezi mzima bila mafanikio. Nipo dar es salaam.
Mwanza inapatikana, tuwasiliane au tembelea website yeti ya mwasenda.org
 
Nashukuru kwa ushauri huu. Nitaufanyia kazi. Pia inaonekana una uzoefu na hii kitu. Unaweza tusaidia hatua za kufanya. Kuanzia upandaji wake, matunzo pamoja na wastani wa kiasi kinacho weza kupatikana. Nashukuru
Azolla kama uyoga, upo uyoga wenye sumu na uyoga wenye virutubisho. Azolla ya baharini ni sumu na ndiyo maana hata samaki hawaili. Ingekuwa haina sumu wala usingeikuta. Kumbuka kuna aina kama tisa za azolla. Endelea kudanganyana mje muwalishe mifugo vitu vya ajabu.
 
Back
Top Bottom