Wafugaji wa broilers huko kwenu soko lipoje?

Wafugaji wa broilers huko kwenu soko lipoje?

Wafugaji wenzangu wa broilers huko kwenu soko lipoje maana huku kwenye ni vilio tupu. Saiv nimeamua kugawa tu kuku maana wanazidi kunitia hasara.
Pole sana jaribu kuchinja unaweka kwenye frigi unauza rejareja au tafuta wauza vipande vijiweni toka nenda kwa wauza chips watakuungisha,sikuizi hatusubir wateja waje lasivyo mfuko wa chakula utakuhusu kila siku...pole
 
pole sana jaribu kuchinja unaweka kwenye frigi unauza rejareja
au tafuta wauza vipande vijiweni
toka nenda kwa wauza chips watakuungisha,sikuizi hatusubir wateja waje lasivyo mfuko wa chakula utakuhusu kila siku...pole
Asante sana. Nimeshajaribu kwenda huko ila pamejaa nauza moja moja kwa nadra sana
 
Sipo DSM mkuu
Nenda sokoni kaombe matenga makubwa kwa wauza kuku (jieleze kiume hata kama ni KE - watakuazima au kukukodisha kwa bei ndogo), weka kuku kwenye tenga - katafute lori zinazorudi Dar zikiwa hazina mizigo, waombe - watakubebea kwa bei ndogo tu ukawauze Dar, utapata faida kidogo kuliko hivyo unavyowagawa bure. Changamoto za biashara kama hizo ndio zinazotofautisha vipato baadae, unayekata tamaa utaporomoka na atayekomaa atasogea.
 
Uko wapi? Mi nina soko la uhakika hata kama una kuku 10k. Ili mradi wawe na vigezo vinavyohitajika. Nipo Dar
Mkuu nisaidie maswaliano yako niweze kujiunga kwenye soko Hilo,Mimimfugaji ninao wana week 2 Sasa bandani
 
Nenda sokoni kaombe matenga makubwa kwa wauza kuku (jieleze kiume hata kama ni KE - watakuazima au kukukodisha kwa bei ndogo), weka kuku kwenye tenga - katafute lori zinazorudi Dar zikiwa hazina mizigo, waombe - watakubebea kwa bei ndogo tu ukawauze Dar, utapata faida kidogo kuliko hivyo unavyowagawa bure. Changamoto za biashara kama hizo ndio zinazotofautisha vipato baadae, unayekata tamaa utaporomoka na atayekomaa atasogea.
Broiler aweza kusurvive safari ya Arusha Dar????
Bora awachinje, aweke kwenye friza!

Atafute wapishi wa masherehe, ila na kwaresima ilishaingia!
 
Arusha ni sehemu ya kitalii,jaribu kutbelea kwa wauza chips,mahotelini migahawani hope utapata pa kuanzia
Mkuu nimeshazunguka sanaa ila kila mtu anakwambia ana mtu wake anae mletea. Pia asilimia nyingi ya hotel za kitalii zinataka kuku kienyeji sio hawa wakizungu.
 
Mkuu nimeshazunguka sanaa ila kila mtu anakwambia ana mtu wake anae mletea. Pia asilimia nyingi ya hotel za kitalii zinataka kuku kienyeji sio hawa wakizungu.
Brother hebu nenda kwa Kiongozi wa Dini ujaribu kuombewa,milango itafunguka tu
 
wamebaki wangapi mpk muda huu mkuu, nikuangalizie soko mahali
 
Back
Top Bottom