Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Mkuu kuna mahali nilikuwa nasoma, wanasema gsd wako kwenye two different lines, kwa maana kuna wale ambao ni "working line" na wengine ni "show line" gsd.

Sasa tofauti ni kwamba hawa show line wanakuwa bred kwa ajili ya mashindano/ maonyesho zaidi na ndo wengi wao wako angulated/ wenye migongo iliyo pinda, hips fupi kama jinsi huyo anavyoonekana.

Kwa upande mwingine hawa working line wanakuwa bred kwa ajili ya kazi kama kulinda na kuchunga mifugo/guard dog kwa maana rahisi ni mbwa wa kazi. Wao migongo yako iko somehow straight compared na hao showline.

Nadhani mwingine anaweza ongezea pia
 
mmmh, mzigo
Mkuu hao mbwa asili yao ni uturuki huko. Kwa Africa wapo Namibia tu kwa sasa waligaiwa kwa wafugaji,sababu kubwa ilikua ni chui na simba walikua wanaua sana mifugo ya wafugaji.Hivyo idadi ya chui na simba walipungua sana Namibia sababu wafugaji nao walianza kuwawinda wawamalize. Lakini toka waletewe hao Anatolian shepherds hakuna chui wala simba anayesogelea zizi kiholela.
 
sijawahi kuwaona wala kuwasikia, wewe umenifungua mzee
 
Very true! Na hao gsd wa show lines wanakua na long coat kulinganisha na working line.
 
Very true! Na hao gsd wa show lines wanakua na long coat kulinganisha na working line.
na wataalam wa wanyama hawa gsd, wanasema gsd pure ana short coat, long coat ni kama cross au Waingereza wanaita alsation
 
kwa wabobezi baadhi yao wanajaribu kusema rangi huwa inachangia.
mfano rangi kahawia/ yenye wekundu, na weusi tii wanadai wana IQ kubwa na nirahisi kufundishika
 
Naomba mnisaidie huyu mbwa n aina gani, namfuga ila sielew tatizo sio mkali kabisa ila akiwa na bifu na mtu hasahau na lazima akimuona amtoe mbio ila ukiwa friend kwake hana shida kabisa
 
Napenda sana mbwa, ni muda gani muafaka (umri wa mbwa) kuanza kunfundisha mbwa? wanafundishwa wapi? na gharama za kumfundisha mbwa mmoja zikoje?
 
Napenda sana mbwa, ni muda gani muafaka (umri wa mbwa) kuanza kunfundisha mbwa? wanafundishwa wapi? na gharama za kumfundisha mbwa mmoja zikoje?
umri mzuri zaidi ni kianzia miezi 4 hadi 6.
kuna watu bonafsi wanatoa mafunzo, pamoja na askari wa vikosi vya mbwa na farasi polisi.

lakini uchukue tahadhari kwa madalali wa mbwa ni hatari sana
 
umri mzuri zaidi ni kianzia miezi 4 hadi 6.
kuna watu bonafsi wanatoa mafunzo, pamoja na askari wa vikosi vya mbwa na farasi polisi.

lakini uchukue tahadhari kwa madalali wa mbwa ni hatari sana

Kuna hatari gani kwa madalali watamuiba mbwa wangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…