Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Mkuu hao wajerumani wanapatikana wapi na kwa bei gani,nimesikia bei zao ni sawa na kujenga nyumba ya chumba kimoja.
 
Mkuu hao wajerumani wanapatikana wapi na kwa bei gani,nimesikia bei zao ni sawa na kujenga nyumba ya chumba kimoja.
karibu mikoa yote wanafuga, inategemea uko mkoa gani?
 
Mkuu baada ya kuona sikusomi nikaamua nizame kwa wataalamu wa hii kitu,napenda kutengua kauli yangu nakukiri uko sahihi
 
usijali na karibu mkuu
Cha kukuongezea tu

Gs asilimia almost 70 % sio pure breed hapa bongo ndo maana unakuta zinauzwa hadi 200,000 ,kwa GS pure inaanzia milion hadi na nusu ya miezi 2 ,ila angalizo nyingi tulizonazo sio pure ilikuijua iliyopure vigezo ni hivi
1.urefu wa miguu ya mbele ni mirefu kuliko ya nyuma,na urefu ni 22-26 chini hadi bega (akiwa na zaidi ya mwaka)

2.masikio yake huwa ni makubwa yaliyosimama wima

3.Mkia wa pure breed huwa ni wenye manyoya mengi sana


4 ,kUNA AINA ZA MBWA KARIBU 200 ila DNA Hudhihilisha kama iko pure au imechanganyia ,hii ni ghali ndo maana inaepukwa ,

HITIMISHO

Breed nyingi kwa bongo zimechakachuliwa hivyo ukiamua kufuata wazohili zuri la biashara jiongeze sana kushauriwa alienishauri aliniuzia GS kwa 200,000 nimemuhoji ndo kaniambia ukweli kuwa yangu sio pure breed akaniambia niangalie masikio yamelala sana akaniambia ingekuwa pure hata laki 9 sichukui.Aidha gs akikua anauzwa hadi 8000 usd ,wazungu wa migodini ndo wateja wakishamuona na vigezo vyote unakulamzigo ilani aghali sana pia kuwalea
 
asante kwa utafiti mzuri.
1. Watu wengi hawafahamu gs
matokeo yake wanauziwa cross breed,
ukiwa na pure ni biashara nzuri sana
hizo sifa ulizotaja pia tumejadili posts
za mwanzoni mwa uzi.
2. kuhusu wateja wako wengi zaidi ya
wazungu.
3. TAHADHARI usinunue gsd toka kwa wazungu kama unategemea kuzalisha, huwa wanachoma sindano kuua uzazi kwani wanaamini mwafrika hawezi kutunza mbwa
 
3 ni kweli kabisa mkuu
 
[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]tulijadili pia hapo juu
 

Ni kweli tupu kuwa GS kachakachuliwa sana. Watu wengi wanaofuga GS hawana elimu hata kidogo kuhusu swala zima la uzalishaji GS.

GS anapandwa na jibwa dume lolote tu unategemea nini??

Kwa upande wangu nimeamua kuachana kabisa na GS nimeamua kufunga Belgian Malinois (BM).

Tofauti kubwa kati ya GS na BM ni umbo la mwili tu na miguu ya nyuma.

BM wana mwili mdogo na miguu ya nyuma iko sawa na ya mbele, kwa hiyo wako na umbo la square.

Sifa ya BM:
-Highly intelligent
-More active kuliko GS
-More energetic than GS
-More agile than GS
-Wavumilivu wa magonjwa
-Low cost maintainance
-Hawachoki kwenye mituringa
-Wako sharp mno
-Walinzi wazuri mno.
-Siyo wazuri ukiwa na watoto wadogo, hapa ndo mahali pekee anapo shine GS. GS yuko friendly sana na watoto.
-BM wanatumiwa na wajeshi zaidi sababu ni wepesi kubebeka na wanajeshi wakiwa wanaruka na parachuti zao. GS mzito mno ndo maana anatumiwa na polisi zaidi.

Swala zima la ulinzi linahitaji mbwa wa kukuamusha zaidi kuliko kung’ata. Mbwa anayebweka akiona adui hana tofauti na Security alarm.

GS yupo dunia zaidi ya miaka 1000 iliyopita, ndo maana kachakachuliwe ile mbaya hasa na hawa waswahili wasiozingatia qualities za ku breed mbwa.

Nina mengi ya kusema ila niishie hapa kwa mwezi huu.

GS nawahurumia sana, siyo pure GS tena ila ni GSKOKO.

Wenye pure GS ni wachache mno sehemu kubwa ni kudanganyana tu.
 
mkuu umekandamiza haswa, asante kwa elimu.
mkuu BM puppies wauzaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…