Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

[emoji190] [emoji240]
Hakuna komando wa njaa.
 
Hatari sana.
 

Attachments

  • Screenshot_20230110-105748_Lite.jpg
    Screenshot_20230110-105748_Lite.jpg
    105.6 KB · Views: 53
Ni link nae mkuu, nahitaji huyu kiumbe
0786 959 856
Huyu jamaa anaitwa Edwin Sarungi.
Yupo Tabora ni mfugaji bora sana wa mbwa.

Mwambie hii namba umepewa na jamaa toka Arusha.
Atakusaidia kukuunga na wafuga mbwa wa Mwanza, jamaa ana mtandao mkubwa.

Kuhusu mfugaji wa Mwanza nimepoteza mawasiliano but ni mangi flani anauza mbwa bei kubwa sana hadi 5m but ni mbwa mbwa kweli
 
Ivi haha ma mbwa NI yamungu kweli au mi utashi WA mwanadamu maana utakuta umbwa lipo ma Sura kama Simba,dubu,chuo,umbwa mwitu mengine body inakuankama ya mbuzi flani yaani NI mbwa ila anafanana na mnyama flan ivi WA porini ebu nisanueni kidogo apo
 
Bongo wapo kweli mkuu hao Malamute?
Mkuu hizo species ni ngumu kuzipata. Juzi hapa kuna jamaa yangu alitaka kununua katoto ka Cane Corso, bei yake tu ni over USD2500 halafu bado hujalipia mambo kibao kama vibali, usafiri n.k

Nadhani kama mtu ana mtaji akaweza ku breed species mbalimbali hapa bongo anaweza kupiga hela.
 
Back
Top Bottom