Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.
Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.
Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.
Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).
Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).
Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.
Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.
Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.
Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.
Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.
Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.
Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.
Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions
[emoji190] [emoji240]