Wafugaji wa njiwa njooni hapa

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Habari wakuu.

Mimi ni mraibu mkubwa wa hawa viumbe sio kuwala ila napenda tu kuwatazama. Kuwala kwa kweli kuwachinja huwa nawaonea huruma, najikuta nashindwa.

Kuna rangi nimeiona nikaipenda nataka kujua ni cross njiwa wa aina gani na aina gani ili nipate hii mbegu.
Niliwahi kujaribu kucross Adidas na chokileti akapatikana kijivu tu. Bila hiyo rangi nyeupe hapo.

 
Kuna njiwa mmoja nilikuanae jogoo, huyu alikua msubufu sana.....
Alikua anapeleka moto iwe asubuhi, mchana, jioni hata nikiwa nimetulia home na wageni. Basi last week palikua na jumuiya pale home, yaani haangalii hata msalaba ulikuepo nyumbani basi awe na adabu. Basi nikaona nimchinje tu maana ananitia aibu hata nikiwa na wageni yeanapeleka moto tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Njiwa wastaarabu mkuu. Kwanza kupandana mara nyingi batini huko. Na wakiwa wawili tu mara nyingi maana huwa wanaoneana wivu mwingine akiona wanapanadana anaenda kuharibu.
 
Nilifuga wakakimbia wote sijui nilikosea wapi
Ulifuga wangapi?

Chakula ulikuwa unawapa? Vp usalama wa banda? Paka shume hafikii?

Ukianza na wawili wafungue ndani hata mwezi mzima kama ni hawa wa kawaida ndio uwaachie.

Kama ni hizi breed nzuri za urembk kama hizi ni heri uwafungie ndani moja kwa moja usiwatoe nje ni rahisi kuibiwa maana bei yao imechangamka.
 
Mkuu unafugia wapi. Naweza kupata mbegu?
 
Utotoni niliwafuga.....
Hadi nikawa Don mtaani, maana ndiye nilikuwa namiliki njiwa wengi.
Ajabu eti, nimeanza form one narudi likizo ya mwezi wa nne nakuta Njiwa wangu wote hawapo, eti wameliwa na Paka.
Bado mpaka leo natafakari ni paka gani aliyejua mimi nipo boarding sipo pale home aende akale Njiwa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…