Wafugaji wagomea mazishi ya mwenzao anayedaiwa kuuawa na Polisi

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
#HABARI:

View: https://www.facebook.com/itvtz/videos/1591165991754927/

Baadhi ya wafugaji jamii wa Wamang'ati pamoja na Wasukuma wanaoishi katika Kitongoji cha Nangorokoro, wilayani Liwale, mkoani Lindi, wamesema hawatamzika mfugaji mwenzao Nyerere Mekaba mwenye umri wa miaka 17 anayedaiwa kuuawa na Askari Polisi kwa kupigwa risasi mgongoni na kutokea tumboni Oktoba 9, 2024, mpaka pale Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega watakapofika kitongoji hicho kutoa tamko la Serikali juu ya askari aliyefanya mauaji ya kijana huyo.

Nchi imeendelea kuwa ya kihuni kweli!​
 
Hivi ni kwamba tupo TANZANIA YETU ILE TULIOJIVUNIA au tupo somalia? Walahi nimekuja kugundua kwanini kuna kuwa na kundi la vijana wanaamua kuingia porini na kuwa waasi
Fikiria kaka yako mdogo wako baba yako mjomba n.k ndio anatandikwa risasi hivo afu kesho unapewa connection ya kuzama msituni ili uje ulipize kisasi utaacha? Kuna mbegu serikali inapanda naona wanaona haioti wanaongeza tena kuipanda upya ipo siku watavuna wanachokipanda kwa sasa
 
💯
 
#HABARI:

View: https://www.facebook.com/itvtz/videos/1591165991754927/

Baadhi ya wafugaji jamii wa Wamang'ati pamoja na Wasukuma wanaoishi katika Kitongoji cha Nangorokoro, wilayani Liwale, mkoani Lindi, wamesema hawatamzika mfugaji mwenzao Nyerere Mekaba mwenye umri wa miaka 17 anayedaiwa kuuawa na Askari Polisi kwa kupigwa risasi mgongoni na kutokea tumboni Oktoba 9, 2024, mpaka pale Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega watakapofika kitongoji hicho kutoa tamko la Serikali juu ya askari aliyefanya mauaji ya kijana huyo.

Nchi imeendelea kuwa ya kihuni kweli!​

Wamangati na wasukuma wanasumbua sana na idadi kuuubwa sana mifugo kwa wakukima mno mno mno......RiP Nyerere mfugaji
 
Back
Top Bottom