Wafumba macho kumsogeza fulani

Wafumba macho kumsogeza fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Mungu hakika jabali
Muumba, Allah, Jalali
Kamuumbia mja akili
Yake pekee si ya wawili

Uko na wako mwandani
Mwanyegezana kitandani
Watazama ute ute kidoleni
Naye mwali aupepea ukuni

Wote mwatazamana usoni
Kwa mahaba wakisi kinywani
Wajua huyo wako maishani
Umemjaza mwilini na rohoni

Kumbe hapo kajaa mwili
Lipo jambo laisumbua akili
Katoka kiroho kaacha mwili
Macho kafumba kahama akili

Wampapasa akijua ni Dani
Wajituma mwenzetu Huseni
Mahabani amsifu D moyoni
Hayo ndiyo sehemu ya sirini

Ya siri yabaki sirini
SItafute kujua ya ndani
Msijegawana majengo asilani
Nyie peaneni peaneni peaneni
 
Back
Top Bottom