Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kampuni ya Kichina inayotengeneza kiwandacha saruji katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo imewafungia wafanyakazi wapatao 60, raia wa nchi hiyo katika eneo la ujenzi tangu mwezi Machi.
Wawakilishi wa kampuni hiyo wanasema uamuzi huo ulichukuliwa ili kuzuwia uwezekano wa wafanyakazi hao kumuambukiza virusi vya corona muajiri wao.
Kiwanda cha saruji cha Salamanga kinajengwa katika wilaya ya Matutuone katika jimbo la Maputo.
Uamuzi huo umewafanya wafanyakazi wawe mbali na familia zao.
Wakili Paulino Cossa anasema hatua hiyo inakiuka sharia za kazi.
Muwakilishi wa kampuni hiyo anameahidi kuwaachilia wafanyakazi hao wiki ijayo.