Wafungwa waliompora silaha Askari, kumjeruhi wakamatwa

Wafungwa waliompora silaha Askari, kumjeruhi wakamatwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limewakamata wafungwa wanne wanaodaiwa kutoroka baada ya kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mwilini mlinzi, Askari Magereza na kumpora silaha.

Wafungwa hao wanadaiwa kumpora bunduki aina ya Uzi-gun yenye namba TZPS 5570-062974 Sajeni Feedolin Madembwe (53) wa gereza la Iringa, mkazi wa Kibwabwa .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, alisema juzi kuwa tukio la wafungwa hao kutoroka lilitokea Novemba 16, mwaka huu, majira ya mchana katika msitu wa Wilolesi, Manispaa ya Iringa, wakati askari huyo akiwasimamia wafungwa kuchanja kuni kwa ajili ya matumizi ya chakula gerezani .

Aliwataja wafungwa hao waliokamatwa kuwa ni Richard Mbondamila (22) mkazi wa Imalutwa, Ilula wilayani Kilolo aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la wizi, Haroun Boniphace (22) mkazi wa Majengo Migoli mkoani njombe aliyekuwa akitumikia kifungo cha miezi saba kwa kosa la kujeruhi wanyama.

Wengine ni Staford Kalinga (20) mkazi wa Mtuwa Ilula, wilayani Kilolo aliyekuwa akitumikia kifungo cha kukutwa na bangi na Isack Kawogo (24) mkazi wa Mgodini, Ramadhani mkoani Njombe aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka minane kwa kosa la kuvunja na kuiba .

Alisema baada ya kupata taarifa za kutoroka, Jeshi la Polisi lilianza msako mkali na usiku wa Novemba 16 majira ya saa 4:00 usiku, waliwakamata Mbiondamila na Boniphace eneo la Gangilonga wakiwa katika jitihada za kutoroka kwenda Iringa mjini. Pia alisema siku ya pili walimkamata Kalinga akiwa eneo la Ndiuka akijaribu kutoroka.

Kamanda Bwire alisema usiku wa kuamkia Novemba 20, Kawogo ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la kiuhalifu kama Mnyapara, aliyepora silaha ya askari magereza, alikamatwa akiwa Njombe na tarifa kamili itatolewa na polisi mkoani humo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Bwire alisema jeshi hilo linajivunia mafanikio makubwa katika kesi ya ubakaji baada ya mwaka 2018 kumkamata Akwino Mtavangu (36) mfanyabiashara mkazi wa Mafinga kwa tuhuma za kubaka mtoto mwenye umri wa miaka sita, mwanafunzi wa darasa la kwanza (jina lake na shule vinahifadhiwa).

Mtavangu anadaiwa kuwa siku ya tukio, alimrubuni mtoto huyo akiwa anatoka shuleni na kumpandisha kwenye pikipiki na kwenda naye nyumbani kwake kisha kumbaka na kumficha kwenye nyumba ambayo haijaisha.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani na Oktoba 19, mwaka huu, katika Mahakama ya MKazi Mkoa wa Iringa, alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela .
 
Yule aliyepora ni mmoja na alipigwa risasi akafa hawa walitoroka baada ya jamaa kora silaha na kumpiga ndugu yake.
 
Kilicho nileta kwenye huu Uzi ni picha nimuone shujaa jambazi,, sasa basi nirudishie MB zangu.
 
Majinga tu hayo, yaani unafanya ujinga wa kupora afu unakamatwa kizembe namna hiyo? Mapori yote hayo
 
Back
Top Bottom