Wafungwa wanaachiwaje jela? Na wakitoka wanaendaje uraiani?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Hivi wafungwa wanaomaliza vifungo vyao huwa wanaachiwaje? Je wanapewa nauli? Na hela ya kuanzia maisha? Au wanafunguliwa mlango na kuambiwa haya nenda uko huru? Wenye uzoefu na HILI watusaidie! Hasa wale waliofungwa vifungo virefu.
 
Kuna jamaa nitamuuliza yeye ni mzoefu na jela, ameenda jela zaidi ya mara saba sasa yaani juzi kuamkia jana ndio amerudi mtaani baada ya kumaliza kifungo cha mwaka mmoja.

Ila kwa jinsi alivyo unaweza kuta muda huu tayari yupo selo za polisi tayari kwa kwenda mahakamani.
 
Rejea maneno ya Nyerere, viboko 12 akiwa anaingia, viboko 12 akiwa anatoka, akamuonyeshe mkewe
 
Hivi wafungwa wanaomaliza vifungo vyao huwa wanaachiwaje? Je wanapewa nauli? Na hela ya kuanzia maisha? Au wanafunguliwa mlango na kuambiwa haya nenda uko huru? Wenye uzoefu na HILI watusaidie! Hasa wale waliofungwa vifungo virefu.
Baada ya kumaliza process zote za mule ndani ikiwemo kupewa vitu vyake alivyoingia navyo kwa maana ya nguo, viatu, kama alikua na big g au pipi mfukoni atavikuta, kama fedha atakabidhiwa....

Lango litafunguliwa askari watamuaga kwa bashasha huku wanamtania na hata wengine kumpa namba zao (hapa inategemea na anayeachiwa kama anajiweza au kapuku) atamkuta mtu/watu waliokuja kumpokea....

Kama hana atatembea mwenyewe kituoni apande bus la kuelekea anapopajua na kama hana fedha na aliishi na wenzie vizuri huko jela ikiwemo askari watampatia nauli ya kumfikisha kwake/kwao....

Kama hana ndugu basi ndio atayaanza maisha ya mtaani rasmi au ataenda nyumba za ibada kuomba msaada au itabidi afanye kosa jipya fasta ili arudi zake jela, kulala bure, kula bure.
 
Acha uongo wewe huwa wanapewa nauli
 
Kuna jamaa nitamuuliza yeye ni mzoefu na jela, ameenda jela zaidi ya mara saba sasa yaani juzi kuamkia jana ndio amerudi mtaani baada ya kumaliza kifungo cha mwaka mmoja.

Ila kwa jinsi alivyo unaweza kuta muda huu tayari yupo selo za polisi tayari kwa kwenda mahakamani.
Ana roho ya jela
 
Kuna dogo tulikuwa naye kitaa alikuwa anasisitiza sana kuwa kule hakufai lakini alikuwa hamalizi mwaka lazima arudi, mara ya mwisho alienda kupiga tukio jeshi la polisi likamtoa kwenye mashindano.
Roho ya jela
 
Nafikiri tarehe ya kutoka inajulikana hivyo ni kukumbusha ndugu, jamaa na marafiki
Si kila alifungwa amtelekezwa, wapo wenye ndugu wa kuwatembelea na kufwatilia taarifa za wapendwa wao huko jela
 
Sio kibongo mfano ccm wanaiba uchaguzi wanataka Kisha mfanye maridhiano wakiwa madarakani.
Kwa nchi zetu afrika haki utaikuta mbinguni tena mawili ni motoni au peponi
Acha fikra za kukaririshwa zoea kujadili mada kama hizi kwa uhuru,usiiruhusu akili yako kuwaza kwa makelele namna hii utapata kisukari Bure. Unadhani kila wakati tukae kujadili CCM na chadema...tuache mambo ya msingi kama haya. Be dynamic ndugu
 
Kwani hupo kwenye serikali ya chama gani!.
Mi nipo kwenye nchi za watu ukiwa mfungwa unapata stahiki yako hata kama walikufunga kilomita 1200 Toka hapo
 
Back
Top Bottom