Wafungwa wanaachiwaje jela? Na wakitoka wanaendaje uraiani?

Wafungwa wanaachiwaje jela? Na wakitoka wanaendaje uraiani?

Hivi mfano mtu akihukumiwa akiwa mjamzito labda 2 months na kuendelea treatment yao huwa ipoje gerezani !! Na akijifungua mtoto anatunzwa vipi maana tunajua mama mjamzito au aliyejifungua anahitahi uangalizi wa karibu.
Je huyo mtoto ataishi gerezani na mama ?
 
Kwa Tanzania naomba unyamaze tu.ndio maana gerezani Siri anaijua mfungwa
 
Baada ya kumaliza process zote za mule ndani ikiwemo kupewa vitu vyake alivyoingia navyo kwa maana ya nguo, viatu, kama alikua na big g au pipi mfukoni atavikuta, kama fedha atakabidhiwa....

Lango litafunguliwa askari watamuaga kwa bashasha huku wanamtania na hata wengine kumpa namba zao (hapa inategemea na anayeachiwa kama anajiweza au kapuku) atamkuta mtu/watu waliokuja kumpokea....

Kama hana atatembea mwenyewe kituoni apande bus la kuelekea anapopajua na kama hana fedha na aliishi na wenzie vizuri huko jela ikiwemo askari watampatia nauli ya kumfikisha kwake/kwao....

Kama hana ndugu basi ndio atayaanza maisha ya mtaani rasmi au ataenda nyumba za ibada kuomba msaada au itabidi afanye kosa jipya fasta ili arudi zake jela, kulala bure, kula bure.
Walioachiwa na Magufuli, waliokuwa wamefungwa maisha au kunyongwa, wengi walirudi gerezani, wengine wakauawa na wananchi, wachache ndo wapo
 
Kuna dogo tulikuwa naye kitaa alikuwa anasisitiza sana kuwa kule hakufai lakini alikuwa hamalizi mwaka lazima arudi, mara ya mwisho alienda kupiga tukio jeshi la polisi likamtoa kwenye mashindano.
Mbona magereza yana minimarkets siki hizi
 
Hivi mfano mtu akihukumiwa akiwa mjamzito labda 2 months na kuendelea treatment yao huwa ipoje gerezani !! Na akijifungua mtoto anatunzwa vipi maana tunajua mama mjamzito au aliyejifungua anahitahi uangalizi wa karibu.
Je huyo mtoto ataishi gerezani na mama ?
Atapata tu special food kama watu wa HIV na TB hua wana special food yao japo haina sana utofauti na chakula cha wengine, akijifungua atakaa na mtoto kwa miezi mitatu/sita ndugu zake wataambiwa wamchukue kama hana ndugu basi atakomaa nae nadhani hadi miaka miwili atapelekwa ustawi wa jamii au kuna askari hua wanawachukua kuwalea (hii ni kwa mapenzi na makubaliano baina yao)

Mule sio sehemu salama kulea mtoto.
 
Walioachiwa na Magufuli, waliokuwa wamefungwa maisha au kunyongwa, wengi walirudi gerezani, wengine wakauawa na wananchi, wachache ndo wapo
Waliofungwa vifungo virefu wengi wakiachiwa ramani inakua ishapotea, wengine wameshasahaulika na ndugu zao, wanaona bora kurudi jela kusubiri kifo au wanarudi kwenye mishe zao wanadakwa wanapigwa kiberiti,

Serikali ingeanzisha tu utaratibu wa kuwapa chochote cha kuanzia pindi watokapo jela, maana ujuzi wanakua wameshaupata jela.
 
Atapata tu special food kama watu wa HIV na TB hua wana special food yao japo haina sana utofauti na chakula cha wengine, akijifungua atakaa na mtoto kwa miezi mitatu/sita ndugu zake wataambiwa wamchukue kama hana ndugu basi atakomaa nae nadhani hadi miaka miwili atapelekwa ustawi wa jamii au kuna askari hua wanawachukua kuwalea (hii ni kwa mapenzi na makubaliano baina yao)

Mule sio sehemu salama kulea mtoto.
Sio salama kweli aseee, maana mtoto anahitaji uangalizi wa karibu !! Tatizo magereza yetu hayaendelezwi yamejengwa vile vile kikoloni sana ! Ilibidi mtu akiwa na hali kama hiyo atengwe kabisa na wengine !!!
 
Au wanafunguliwa mlango na kuambiwa haya nenda uko huru? Wenye uzoefu na HILI watusaidie! Hasa wale waliofungwa vifungo virefu.
Wanaachiwa baada ya kusaini documents za kuachiwa na wanaenda kuzisaini magereza sio Mahakamani pale akisomewa hukumu kua ameachiwa huru ataambatana na Bwana jela Askari magereza kwenye ngarangara na wafungwa na mahabusu wengine mpaka magereza kule ataenda kuaga wafungwa wenzake na mahabusu kisha kurudisha na kuchukua vinavyomhusu kisha anasaini fomu ya kuachwa huru inayobaki km record huko magereza

Ndio maana mfungwa akiachiwa Mahakamani akaanza kuondoka bila kufuata utaratibu Askari magereza wanamkamata mara moja maana lazima aende kusaini paper za kuachiwa huru kule magereza Kisha kukabidhi chochote kinachohusu magereza na yeye kukabidhiwa kinachomhusu baada ya hapo anaachwa huru

Kuhusu nauli wanaangalia umbali anakoenda wanampatia nauli arudi kwao au ikiwezekana anabebwa na Gari la magereza na kurudishwa kwao, mfungwa ni mteja wa magereza km alivyo mgonjwa mteja wa hospitali
 
Sio salama kweli aseee, maana mtoto anahitaji uangalizi wa karibu !! Tatizo magereza yetu hayaendelezwi yamejengwa vile vile kikoloni sana ! Ilibidi mtu akiwa na hali kama hiyo atengwe kabisa na wengine !!!
Kutengwa ni ngumu kwa magereza zetu hizi tena watu walivyovurugwa huko hakuna mtu anajali,

Kuna wengine wanaingia wazima, wanapatia mimba humo humo ndani, jiulize how [emoji28]
 
Hivi wafungwa wanaomaliza vifungo vyao huwa wanaachiwaje? Je wanapewa nauli? Na hela ya kuanzia maisha? Au wanafunguliwa mlango na kuambiwa haya nenda uko huru? Wenye uzoefu na HILI watusaidie! Hasa wale waliofungwa vifungo virefu.
Kuna michakato huanza mwezi ama wiki mmoja kabla
1. Kuwatafuta na Kuwajulisha ndugu na marafiki ukomo wa kifungo
2. Kupata nasaha za bwana jela
3. Maandalizi ya kurejea uraiani
4. Kwa wenye vifungo vya muda mrefu na waliopoteza mawasiliano na ndugu na jamaa zao magereza huwasaidia nauli na sometimes chochote cha kuanzia maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutengwa ni ngumu kwa magereza zetu hizi tena watu walivyovurugwa huko hakuna mtu anajali,

Kuna wengine wanaingia wazima, wanapatia mimba humo humo ndani, jiulize how [emoji28]
Hizi ni mimba za maaskari sasa na Bwana Jela au huwa kuna magereza wanachanganywa wafungwa wa kike na wa kiume ? Halafu muhuni anakana mtoto
 
Dada Dream Queen vipi magereza ya watoto yapo hapa kwetu kweli ? Je madogo wakifungwa vipi kuhusu kuendeleza ndoto zao labda kwa wanaosoma shule huwa wanaendelezwa ? Mfano dogo anafungwa akiwa std six ? Labda alifungwa ana miaka 14 akifikisha umri wa utu uzima utaratibu wake ukoje ?
 
Nafikiri tarehe ya kutoka inajulikana hivyo ni kukumbusha ndugu, jamaa na marafiki
Si kila alifungwa amtelekezwa, wapo wenye ndugu wa kuwatembelea na kufwatilia taarifa za wapendwa wao huko jela
Kuna wale wenye namba ndefu hivyo mpaka kumaliza kifungo anaweza akarotate magereza kadhaa akitumikia adhabu. So ikitokea kapata msamaha wa Rais atachomokea kulekule alipo. Kwakuwa bwana jela anakuwa na faili lake so atampa release note na warrant itasoma mpaka destination makwao.

Ni jitihada za mfungwa kuwasiliana na nduguze ndo zitakazofanya ndg wajue yupo gereza lipi.
Huko magerezani wapo wafungwa wengi washapoteza mawasiliano na ndg zao. Hasa wale wenye namba ndefu na kuhamishwa mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom