Wagagagigikoko ni watu wa wapi?

Wagagagigikoko ni watu wa wapi?

Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chonya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, Dkt. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
Hapo kwa Nanga nimecheka sana...sijawahi kuona au kusikia MTU mjinga kama chief hata kama ni wa imagination.
 
Me najua wagagagigilikoko ni majirani wa wapastiko enzi na umslopagazi alipokuwa na inkosikazi yake
 
Uko SAWA kabisa Ndugu yangu. Dhumuni la safari ni KUTEMBEA/Mapuziko wakati wa Likizo. Ni kweli walitumia Jahazi. Walipo pata dhoruba, Bulicheka na Mkewe Elizabeth waliokoka kwa kuelea juu ya Meza. Wengine wote waliangamia. Walitua katika Kisiwa. Hapakuwa na makazi ya Watu. Waliogopa wanyama wakali. Walitengeneza nyumba yao kwa kujenga kati ya Minazi 4 ilokuwa karibu karibu. Walitumia meza yao kama "msingi" wa nyumba yao, na makauti kama paa. Nyumba ilikuwa juu kama kiota cha ndege mkubwa. Siku za mwanzo walikula chakula kidogo walicho okoka nacho, pamoja na madafu na nazi. Kuwa wakati Bulicheka alienda kuwinda, akamwua Mbuni kwa staili ya ajabu.
Ilitokea siku moja Mfalme (wa Bara) aitwae Huihui alitembelea kisiwa kile. Ilkuwa sehemu ya miliki yake. Alishangazwa na kiota kile cha ajabu. Akaawamuru wasaidizi wake kakaonewakaangalie kuna nini. Alishangaa zaidi kumwona Binadamu anaishi mle. Alimwamuru ashuke, Bulicheka akakataa. Akasema kama kweli Huihui anataka amani, WAPIGANE.....(inaendelea zaidi)...
Chuwaalbert,
Asante kwa uelewa wako kuhusu Hadithi za kale,pia fasihi yako ni ya kisomo sio ya kuokota barabarani napendekeza kama si mwalimu jitahidi uwe mmoja kwa wakati wako Wa ziada.

Nasikitika nimekutana na nyuzi hii wakati umepita hivyo nimeikumbushia tu ikiwa wachangiaji bado wapo tuendelee nayo.
Hadithi hizo mlizo zielezea na watu mliowataja zinapatika katika kotabu cha Someni kwa furaha kitabu cha 3B, Huihui na wagagagigikoko, Bulicheka na Elizabeth, Karume kenge hutaki kwenda shule unapenda kuwinga Kuku nk.

Kipindi cha vitabu hivi kilifundisha wasomaji mambo mengi ambayo mengi yalikuwa ubunifu tu hadithi, majina na nyimbo, kwa kumbukumbu ndogo nakumbuka series ya vitabu hivi niliovyovisoma Mimi kati ya mwaka 64 na 66 ni someni kwa Furaha kitabu cha , 3, 3B na cha 4 kilichokuwa na Hadithi ya Sultan Tarabushi.

Kipindi hiki kilitawaliwa na waandishi mahiri kama Shaban bin Robert alieandika viatabu Vingi kama:-
1.Maisha yangu
2. Kusadikika
3. Sinti Bint Saad
4. Adili na nduguze
5. Nchi za Ugaibuni
Na vingine Vingi ambavyo Vilikuwa katika Syllabus ya kiswahili elimu ya msingi mpaka kuendelea Secondari.

Wakati huo kulikuwa na hadithi nyingi zilizowavitia sana wasomaji Wa kiswahili, Alfu lela Ulela au siku Elfu na moja kitabu cha 1 - 8...Aladin na taa ya ajabu, Zimwi mla watu, Sindbad baharia nk.

Waandishi ka Reader Hahard na kitabu chale cha Alan Qiarterman na shoka lake la ajabu Inkoskazi, utaona huu no ubunifu waandishi Wa wakati ule.

Ni jambo la kusikitisha kuona taasisis ya elimu ilipuuza vitabu hivi na kuleta vitabu vya Abel mwanga kitu kilichopelekea upeo Wa wanafunzi katika kiswahili kushuka.
Lingelikuwa jambo zuri kama waliweka suplimentary exercises kwa vitabu hivi kwa wanafunzi Wa secondary katika kuimarisha Kiswahili.
 
oooh wataka kuniambia haya ni yakubuni na hakuna anayejua

Hayo majina na makabila yaliandikwa kwenye kitabu cha Kiswahili ambacho tulikisoma darasa la tatu 1966.

Bulicheka na mkewe Lizabeta wa kabila la Wagagagigikoko.

Kalumekenge alipokataa kwenda shule.

Bibi tarabushi.

Maneno haya ni magumu kwa mtoto wa darasa la tatu. Hebu fikiria neno Wagagagigikoko mpaka uweze kulisoma sawasawa ilibidi ujipinde kweli kweli.

Vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa ‘Someni kwa furaha’ na kweli tulifanya hivyo maana mpaka leo tunazikumbuka hizo hadithi.

Nakumbuka pia vilikuwepo vya kiingereza Oxford English books for African students.
Humo mulikuwa na hadithi kama:
My name is Shokolokobangoshei
Juma Saidi the lorry driver
Abdul and the king
Mr and Mrs Mutabingwa....

Hakika tukisoma kwa furaha.
 
Kitabu kiliitwa tu Bulicheka

Mke wa Bulicheka aliitwa Elizabetha

Safari yao haikuwa na dhumuni lolote isipokuwa kutalii tu

Baada ya merikebu kupigwa dhoruba waliokoka kwa kudandia meza iliyokuwa ikielea

Walipofika nchi kavu ni meza hiyo waliitumia kujenga nyumba kwenye minazi minne iliyokaribiana

Alipokwenda kuwinda akiwa anaburuza windo lake (mbuni) Kurudi nyumbani akashtukia windo limeshamezwa na mamba mwili mzima mpaka shingo aliyoshika

Akatoka nduki kufika nyumbani mke hayupo katika kumsaka ndio akakutana na kabila la wagagagigikoko chini ya mfalme huihui.

Akaishi na watu hao, siku moja mvua kubwa ikanyesha mwamba wa ukuta wa nyumba ukapasuka pesa nyingi sana zikamwagika toka ukutani akafurahi akapakia magunia kwa magunia


Hapa ni mwisho wa story kwa dondoo lakini alirudi kwao

nYaNi wA KaLe

Hiyo ya mamba na ukuta kutoka pesa sijawahi kusikia kabla.
 
Ngwango

Yule mwandishi nadhani jina lake ni H. Rider Haggard ambaye alitunga vitabu kama King Solomons mines na Allen Quartermain.

Humo ndiyo unamkuta Umslopogaas na shoka lake Inkosikazi.

Nakumbuka kulikuwa na msemo ‘pigo moja pigo takatifu la inkosikazi’

Vijana someni vitabu.
 
Ngwango

Yule mwandishi nadhani jina lake ni H. Rider Haggard ambaye alitunga vitabu kama King Solomons mines na Allen Quartermain.

Humo ndiyo unamkuta Umslopogaas na shoka lake Inkosikazi.

Nakumbuka kulikuwa na msemo ‘pigo moja pigo takatifu la inkosikazi’

Vijana someni vitabu.
Mkuu,
Uko sahihi kabisa about H. Ridder Haggard lakini hatuwezi kukumbuka yote maana muda umepita ni mrefu unaenea umri Wa mtu mwenye wajukuu.
Kwa kuwajuza tu vitabu hivyo vinapatikana maeneo ya Accra na City Fire niliwaihi kununua Hekaua za Abunuasi original.
 
Hayo majina na makabila yaliandikwa kwenye kitabu cha Kiswahili ambacho tulikisoma darasa la tatu 1966.

Bulicheka na mkewe Lizabeta wa kabila la Wagagagigikoko.

Kalumekenge alipokataa kwenda shule.

Bibi tarabushi.

Maneno haya ni magumu kwa mtoto wa darasa la tatu. Hebu fikiria neno Wagagagigikoko mpaka uweze kulisoma sawasawa ilibidi ujipinde kweli kweli.

Vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa ‘Someni kwa furaha’ na kweli tulifanya hivyo maana mpaka leo tunazikumbuka hizo hadithi.

Nakumbuka pia vilikuwepo vya kiingereza Oxford English books for African students.
Humo mulikuwa na hadithi kama:
My name is Shokolokobangoshei
Juma Saidi the lorry driver
Abdul and the king
Mr and Mrs Mutabingwa....

Hakika tukisoma kwa furaha.
Wakuu,
Msipate shida ya kuelezaaa tu na mifano ipo vitabu hivyo hapo
 

Attachments

  • images (29).jpeg
    images (29).jpeg
    9.8 KB · Views: 12
  • images (28).jpeg
    images (28).jpeg
    7.6 KB · Views: 9
  • images (27).jpeg
    images (27).jpeg
    13.3 KB · Views: 9
May 26, 2011
Wiki kadhaa zilizopita, nikiwa Madison, katika mkutano wa Peace Corps, niliingia katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison. Nilifurahi kuingia katika maktaba hii, ambayo niliizoea wakati nasoma katika chuo hicho, 1980-86.

Niliangalia vitabu vya ki-Swahili, ambavyo ni vingi katika maktaba hii, nikavutiwa na vitabu vya Someni Kwa Furaha, tulivyosoma tulipokuwa shule ya msingi.

Nilijikumbusha kuhusu Bulicheka na mke wake Lizabeta, Wagagagigikoko na mfalme wao, Makari Hodari, Kalumekenge, na Pauli mwenye mikono michafu.

Tulibahatika, enzi za utoto wetu, kuwa na vitabu vya kusisimua, vilivyotupa motisha ya kusoma. Vitabu hivi viliandikwa kuzingatia umri wetu. Walimu walikuwa makini, katika kufundisha, kwa mbinu mbali mbali, kama vile nyimbo. Tuliimba alfabeti hadi orodha. Nawasifu na kuwashukuru waalimu wale

Soma zaidi kwa hisani kubwa ya Source :
 
Padri Alfons Loogman nguli wa lugha ya kiSwahili, mtunzi mbobezi wa vitabu vya hadithi vyenye wahusika kama Wagagagigikoko na mfasiri wa vitabu walivyosoma watoto wa zamani.

Listi ya vitabu 19 alivyotunga au kuvitafsiri inapatikana kwa kubofya linki hii : Encore -- a:(loogman alfons)
  1. Usingizi, ndoto na jinamizi / Alfons Loogman​

    Someni bila shida / Alfons Logman​

    Safari za Bwana Henri Morton Stanley / A. Loogman​

    Someni kwa furaha / A. Loogman​

Biografia (historia ya maisha) ya Padri Alfons Loogman kwa ufupi hapa chini:

Fr. Alfons Loogman, C.S.Sp.

Loogman_teaching.jpg

Photo courtesy of the University Archives & Special Collections, Gumberg Library, Duquesne University

Born in 1897 in the Netherlands, Alfons Loogman was a Spiritan priest who became an expert in Swahili.

He was a missionary, writer, painter, and teacher. He studied at the Jesuit College of St. Ignatius in Amsterdam, and at the Collegium Maximum at Louvain. After joining the Congegation of the Holy Spirit, he was sent in 1922 to Africa.

He spent 11 years as the pastor at the Spiritan mission in Mombasa, Kenya. Loogman was the founder of the first Catholic newspaper in Swahili, and he was the founder of a new parish in Makupa, building a church there.

It was during his time at Makupa that he discovered his gift for languages and became expert in Swahili. In 1937, he was given the task of organizing a seminary in Morogoro, Tanganyika, where he taught until 1956.

Due to sickness, in 1959 Fr. Loogman was forced to leave Africa. He came to Duquesne University, where he taught Swahili for the University’s African Institute. It was while at Duquesne that he wrote his most important work, a grammar of Swahili.

A prolific author, he also wrote many works to assist those studying Swahili, as well as translating the New Testament and The Imitation of Christ into that language. Due to health reasons he was forced to resign his position at Duquesne. He died in 1964 at the age of 67 while on a visit to the Netherlands.

To honor Fr. Loogman, the Center for African Studies offers the Loogman Grants for Duquesne faculty who are interested in pursuing research interests in Africa
Source : LibGuides: Swahili: Fr. Alfons Loogman
 
December 19, 2011
Kwa sisi tuliosoma shule ya msingi zamani, Makari Hodari ni jina tunalolikumbuka sana. Tulisoma habari zake zilizotungwa na Padri Alfons Loogman, mwandishi wa vitabu vya Someni Bila Shida na Someni Kwa Furaha. Kwa kweli, padri huyu aliziteka nyoyo zetu watoto, akatufanya tupende kusoma. Aliandika vitabu kadhaa vya masomo ya ki-Swahili na hata mwongozo kwa walimu kuhusu kufundisha kusoma.
Nakumbuka kuwa katika shule yangu ya msingi ya Litembo, tulikuwa tunasoma hadithi ya Makari Hodari kwa kuiimba. Watoto wote darasani tulikuwa tunaimba kwa pamoja, kwa furaha. Hadi leo naweza kuimba tulivyoimba. Na mwalimu alikuwa akiimba nasi. Pamoja na utamu wa hadithi, tulivutiwa na picha.

Nikiitafakari hadithi ya Makari Hodari, naona kuwa ilijengeka katika mfumo wa zile hadithi za kale za mashujaa, ambazo zinasimuliwa katika tamaduni mbali mbali. Kwa mfano, Wa-Haya wana hadithi za mashujaa kama Mugasha, Rukiza, na Kilenzi. Wa-Chagga wana hadithi ya Mrile, wa-Swahili hadithi ya Liongo Fumo. Hadithi ya Makari Hodari imerahisisha na kufupisha masimulizi ili yawavutie watoto kwa umri wao. Lakini inataja vitendo vya ushujaa, majigambo, na nafasi ya mama katika maisha ya shujaa.

Leo ni mara ya pili kwangu kuandika kuhusu vitabu hivi vya Padri Loogman katika blogu hii. Nilipoandika mara ya kwanza, ujumbe wangu uliwafikia watu wengi, hasa baada ya kutokea katika blogu ya Michuzi. Leo nimeona niwaletee wadau hadithi ya Makari Hodari, waione pia picha yake na picha ya mama yake

Source: kwa hisani kubwa ya : Makari Hodari
 
Mwenye kujua kabila hili chimbuko lake ni wapi anijuze mana nimesikia walikuwa na mfalme aliyeitwa Huihui au mfalme Juha! Wanatoka maeneo gani hapa Tanzania. Nahitaji kujua historia yao kidogo.


Usihangaike kutafuta; wagagagigikoko wako Kenya!

Kwa sababu Bulicheka alikuwa mwalimu wa shule ya Kilakala (ambayo iko Morogoro Tanzania). Siku moja akamwambia mke wake Lizabeta kuwa twende tusafiri kuiona dunia. Mke wake yule akakataa na kusema ukitaka kusafiri kuiona dunia nzima nenda peke yako, mimi siendi. Baada ya mashauriano wakakubali kuwa watafunga safari kwenda Mombasa, Lamu, Aden hadi Uarabuni. Sasa wakiwa wanakaribia Mombasa, meli yao ikapatwa na dharuba, na hapo ndipo Wagagagigikoko waliwaotokea!

Kwa hiyo utakubaliana nami kuwa Wagagagigikoko wako Kenya karibu na Mombasa; huenda bado wapo hadi leo.

Kitabu kiliitwa tu Bulicheka

Mke wa Bulicheka aliitwa Elizabetha

Safari yao haikuwa na dhumuni lolote isipokuwa kutalii tu

Baada ya merikebu kupigwa dhoruba waliokoka kwa kudandia meza iliyokuwa ikielea

Walipofika nchi kavu ni meza hiyo waliitumia kujenga nyumba kwenye minazi minne iliyokaribiana

Alipokwenda kuwinda akiwa anaburuza windo lake (mbuni) Kurudi nyumbani akashtukia windo limeshamezwa na mamba mwili mzima mpaka shingo aliyoshika

Akatoka nduki kufika nyumbani mke hayupo katika kumsaka ndio akakutana na kabila la wagagagigikoko chini ya mfalme huihui.

Akaishi na watu hao, siku moja mvua kubwa ikanyesha mwamba wa ukuta wa nyumba ukapasuka pesa nyingi sana zikamwagika toka ukutani akafurahi akapakia magunia kwa magunia


Hapa ni mwisho wa story kwa dondoo lakini alirudi kwao

nYaNi wA KaLe
Mke wa Bulicheka alikuwa anaitwa Lizabeta, siyo Elizebetha
 
Mkuu,
Uko sahihi kabisa about H. Ridder Haggard lakini hatuwezi kukumbuka yote maana muda umepita ni mrefu unaenea umri Wa mtu mwenye wajukuu.
Kwa kuwajuza tu vitabu hivyo vinapatikana maeneo ya Accra na City Fire niliwaihi kununua Hekaua za Abunuasi original.

Wewe ni mzee mwenzangu tuko age group moja.

Usijali hapa ni tunakumbushana tu kwani ni kweli miaka mingi sana imeshapita.
 
Wewe ni mzee mwenzangu tuko age group moja.

Usijali hapa ni tunakumbushana tu kwani ni kweli miaka mingi sana imeshapita.
Wewe ni mzee mwenzangu tuko age group moja.

Usijali hapa ni tunakumbushana tu kwani ni kweli miaka mingi sana imeshapita.
Bitimkongwe,
Nashukuru kwa habari njema kuhusu umri bana, wanasema Old is Gold tunapaswa thamini tulipofika. Hongera!
 
Back
Top Bottom