born again pagan
JF-Expert Member
- Apr 28, 2014
- 2,336
- 1,491
Hapo kwa Nanga nimecheka sana...sijawahi kuona au kusikia MTU mjinga kama chief hata kama ni wa imagination.Hao ni KABILA na Mfalme aliyekuwa kwenye FIKRA za Msanii. Mwana Fasihi aliifasili na kuisawili Jamii. Ni Kama OKONKWO na Umuofia yake. Ki Uhalisia, Wahusika, maeneo na hata matukia ambayo ni kazi ya sanaa ni UBUNIFU. Ila kazi ya Sanaa IKIKUBALIKA, huchukuliwa na hadhira kama ni UKWELI... Rejea pia kazi za Fasihi kama za Musiba (na Willy Gamba wake), Xuma, JORAM KIANGO, Chonya wa Chilonwa, Lorienka Lenkaken, Obierika, Njoroge, Dkt. Stokimani, Honorable Chief Alhaj Dr. Nanga, MP.... na wengine wengi....
Chuwaalbert,Uko SAWA kabisa Ndugu yangu. Dhumuni la safari ni KUTEMBEA/Mapuziko wakati wa Likizo. Ni kweli walitumia Jahazi. Walipo pata dhoruba, Bulicheka na Mkewe Elizabeth waliokoka kwa kuelea juu ya Meza. Wengine wote waliangamia. Walitua katika Kisiwa. Hapakuwa na makazi ya Watu. Waliogopa wanyama wakali. Walitengeneza nyumba yao kwa kujenga kati ya Minazi 4 ilokuwa karibu karibu. Walitumia meza yao kama "msingi" wa nyumba yao, na makauti kama paa. Nyumba ilikuwa juu kama kiota cha ndege mkubwa. Siku za mwanzo walikula chakula kidogo walicho okoka nacho, pamoja na madafu na nazi. Kuwa wakati Bulicheka alienda kuwinda, akamwua Mbuni kwa staili ya ajabu.
Ilitokea siku moja Mfalme (wa Bara) aitwae Huihui alitembelea kisiwa kile. Ilkuwa sehemu ya miliki yake. Alishangazwa na kiota kile cha ajabu. Akaawamuru wasaidizi wake kakaonewakaangalie kuna nini. Alishangaa zaidi kumwona Binadamu anaishi mle. Alimwamuru ashuke, Bulicheka akakataa. Akasema kama kweli Huihui anataka amani, WAPIGANE.....(inaendelea zaidi)...
oooh wataka kuniambia haya ni yakubuni na hakuna anayejua
Kitabu kiliitwa tu Bulicheka
Mke wa Bulicheka aliitwa Elizabetha
Safari yao haikuwa na dhumuni lolote isipokuwa kutalii tu
Baada ya merikebu kupigwa dhoruba waliokoka kwa kudandia meza iliyokuwa ikielea
Walipofika nchi kavu ni meza hiyo waliitumia kujenga nyumba kwenye minazi minne iliyokaribiana
Alipokwenda kuwinda akiwa anaburuza windo lake (mbuni) Kurudi nyumbani akashtukia windo limeshamezwa na mamba mwili mzima mpaka shingo aliyoshika
Akatoka nduki kufika nyumbani mke hayupo katika kumsaka ndio akakutana na kabila la wagagagigikoko chini ya mfalme huihui.
Akaishi na watu hao, siku moja mvua kubwa ikanyesha mwamba wa ukuta wa nyumba ukapasuka pesa nyingi sana zikamwagika toka ukutani akafurahi akapakia magunia kwa magunia
Hapa ni mwisho wa story kwa dondoo lakini alirudi kwao
nYaNi wA KaLe
Me najua wagagagigilikoko ni majirani wa wapastiko enzi na umslopagazi alipokuwa na inkosikazi yake
Mkuu,Ngwango
Yule mwandishi nadhani jina lake ni H. Rider Haggard ambaye alitunga vitabu kama King Solomons mines na Allen Quartermain.
Humo ndiyo unamkuta Umslopogaas na shoka lake Inkosikazi.
Nakumbuka kulikuwa na msemo ‘pigo moja pigo takatifu la inkosikazi’
Vijana someni vitabu.
Wakuu,Hayo majina na makabila yaliandikwa kwenye kitabu cha Kiswahili ambacho tulikisoma darasa la tatu 1966.
Bulicheka na mkewe Lizabeta wa kabila la Wagagagigikoko.
Kalumekenge alipokataa kwenda shule.
Bibi tarabushi.
Maneno haya ni magumu kwa mtoto wa darasa la tatu. Hebu fikiria neno Wagagagigikoko mpaka uweze kulisoma sawasawa ilibidi ujipinde kweli kweli.
Vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa ‘Someni kwa furaha’ na kweli tulifanya hivyo maana mpaka leo tunazikumbuka hizo hadithi.
Nakumbuka pia vilikuwepo vya kiingereza Oxford English books for African students.
Humo mulikuwa na hadithi kama:
My name is Shokolokobangoshei
Juma Saidi the lorry driver
Abdul and the king
Mr and Mrs Mutabingwa....
Hakika tukisoma kwa furaha.
Duhbulicheka ni nani???!
Zephta,
Nadhani asili yao ni Kyelawagangagikoko sio watu wa Iringa na Songea songea huko?
Biografia (historia ya maisha) ya Padri Alfons Loogman kwa ufupi hapa chini:
Usingizi, ndoto na jinamizi / Alfons Loogman
Someni bila shida / Alfons Logman
Safari za Bwana Henri Morton Stanley / A. Loogman
Someni kwa furaha / A. Loogman
Nakipataje mwalimuJe, umesha wahi kusoma kitabu (hadithi) ya Safari za Bulicheka? Kma bado NAPENDEKEZA ukitafute na kukisoma. Ni kizuri...
Mwenye kujua kabila hili chimbuko lake ni wapi anijuze mana nimesikia walikuwa na mfalme aliyeitwa Huihui au mfalme Juha! Wanatoka maeneo gani hapa Tanzania. Nahitaji kujua historia yao kidogo.
Mke wa Bulicheka alikuwa anaitwa Lizabeta, siyo ElizebethaKitabu kiliitwa tu Bulicheka
Mke wa Bulicheka aliitwa Elizabetha
Safari yao haikuwa na dhumuni lolote isipokuwa kutalii tu
Baada ya merikebu kupigwa dhoruba waliokoka kwa kudandia meza iliyokuwa ikielea
Walipofika nchi kavu ni meza hiyo waliitumia kujenga nyumba kwenye minazi minne iliyokaribiana
Alipokwenda kuwinda akiwa anaburuza windo lake (mbuni) Kurudi nyumbani akashtukia windo limeshamezwa na mamba mwili mzima mpaka shingo aliyoshika
Akatoka nduki kufika nyumbani mke hayupo katika kumsaka ndio akakutana na kabila la wagagagigikoko chini ya mfalme huihui.
Akaishi na watu hao, siku moja mvua kubwa ikanyesha mwamba wa ukuta wa nyumba ukapasuka pesa nyingi sana zikamwagika toka ukutani akafurahi akapakia magunia kwa magunia
Hapa ni mwisho wa story kwa dondoo lakini alirudi kwao
nYaNi wA KaLe
Mkuu,
Uko sahihi kabisa about H. Ridder Haggard lakini hatuwezi kukumbuka yote maana muda umepita ni mrefu unaenea umri Wa mtu mwenye wajukuu.
Kwa kuwajuza tu vitabu hivyo vinapatikana maeneo ya Accra na City Fire niliwaihi kununua Hekaua za Abunuasi original.
Wewe ni mzee mwenzangu tuko age group moja.
Usijali hapa ni tunakumbushana tu kwani ni kweli miaka mingi sana imeshapita.
Bitimkongwe,Wewe ni mzee mwenzangu tuko age group moja.
Usijali hapa ni tunakumbushana tu kwani ni kweli miaka mingi sana imeshapita.