Waganda wamechoka, wameingia barabarani, walikua wanatucheka enzi zetu za mapambano, haya wapambane

Waganda wamechoka, wameingia barabarani, walikua wanatucheka enzi zetu za mapambano, haya wapambane

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Waganda wamefikia kikomo, uvumilivu umewazidi, wamechoka udhalimu na manyanyaso, wameingia barabarani na kuandamana na kama ilivyo kawaida ya polisi wa Kiafrika, wamejibu kwa risasi na mabomu ya machozi, mpaka sasa raia saba wameuawa na wengine 45 kujeruhiwa.

Nafahamu fika wanachopitia wenzetu maana binafsi nilihusika kwenye mapambano ya kuleta mabadiliko kwetu hapa Kenya, tulichezea virungu, risasi na mabomu lakini tukakomaa, majirani wote walituona wajinga, ila leo tunajivunia uhuru na ukuaji wa kiuchumi zinazokwenda sambamba, maana lazima ziwepo zote ili haki kwenye nchi itamalaki.

Ni kweli hatujafika tulikokusudia, ila kwa walioishi enzi zile tukilinganisha na ilivyo leo, kuna tofauti kubwa sana na kwa kweli tulivuna tulichofukia au kupanda. Nawatakia kila la kheri Waganda, komaeni tu huko na kwa namna fulani Museveni na wapambe wake watachoka na kuhema na kukubali maridhiano na uboreshwaji wa mifumo ya kiutawala na dola, halkadhalika hata katiba.

---------------------------------

Seven people died and at least 45 were injured in protests that erupted after police arrested Ugandan presidential candidate and pop star Bobi Wine on Wednesday, Ugandan police said.

“As of yesterday evening we had seven people who lost their lives, about 45 people got injuries including an LDU [armed civilian force] whose head was smashed,” police spokesperson Fred Enanga said.

Mr Enanga claimed the National Unity Platform (NUP) led by Wine, who is also a lawmaker, violated election guidelines issued to contain the spread of Covid-19 .

The MP is currently detained at in Jinja following his arrest in Luuka where he had gone to campaign on Wednesday.

“But it (NUP) doesn’t have control over these demonstrators. They don’t have the ability to restore a situation that has gone out of hand and yet they’re promoting violence. This is unacceptable,” Mr Enanga told state-owned Uganda Broadcasting Corporation (UBC) on Thursday morning.

Wine was arrested alongside Jinja-based pastor Andrew Muwanguzi and five other supporters. They are currently being interrogated on charges of negligent conduct likely to spread the infectious disease, obstruction and holding unauthorised assembles.

Police said they had also recorded other crimes of looting, vandalism and robbery by other criminals taking advantage of the violent demonstrations.

Uganda Red Cross said Wednesday evening that their response team had rescued over 30 people from the riots and referred them to different health facilities

Wine was most recently arrested on November 3 moments after registering his candidacy for the January 14 2021 presidential election, over accusations he was planning an illegal rally.

Wine, nicknamed the "Ghetto President", has faced escalating police harassment since announcing his intention to challenge Museveni, who seized power at the head of a rebel army in 1986.

His catchy pop songs about social justice, poverty and corruption have shaken the ruling party and its ageing patriarch Museveni, who at 76 is the only president most Ugandans have ever known.

Huyo Bobi labda ndiyo Mpinzani hapa kwetu kuna Bobi wanna be tundu anaishi Ulaya anakuja siku ya Kampeni na tiketi ya kurudia halafu anawaambia Watanzania waingie barabarani, Watanzania siyo wajinga hivyo, waache hao Wakenya na Waganda wapigane risasi ili kufika waendapo sisi tumechagua nja nyingine.
 
Bob kunyanyua walalahoi waingie road ni rahisi sana maana anashare nao kipigo, na hata kuwekwa mahabusu.

Hawa wanaharakati wa tz au Kenya ni matapeli tu, nashangaa kwanini wakenya wanakuwa wajinga kung'amua mapema tu.

Ona rutto kitu amenza kufanya[emoji51][emoji51][emoji51]
 
Huyo Bobi labda ndiyo Mpinzani hapa kwetu kuna Bobi wanna be tundu anaishi Ulaya anakuja siku ya Kampeni na tiketi ya kurudia halafu anawaambia Watanzania waingie barabarani, Watanzania siyo wajinga hivyo, waache hao Wakenya na Waganda wapigane risasi ili kufika waendapo sisi tumechagua nja nyingine, ...
Umechagua njia gani dada? Umechagua wewe na nani? Halafu uzi wako wa Tulampu umeukimbia kule [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Africa bara la giza. Waandamane tu tuone kama Museveni atawaua wote.
 
2022 kierehere chako cha kupost naomba kiendelee....

umetoka TZ now upo UG ikifika zamu yenu usitukimbie tafadhali at least tukikuona humu tutajua huyu mkenya bado anapumua
 
Aisee, naona mataga wana hasira sana na Bobbi Wine, zaidi hata ya M7. Wanatamani wao ndio wangekuwa IGP wa Uganda. [emoji1]
 
Comment yangu ni ya nne, kasome nilichoandika.

Ulichomekea yale huwa mnakaririshwa Lumumba kisha ukatoweka, rudi uone jamaa wameachia nondo za uhakika uzi unachezea kurasa kadhaa sasa, Mataga wote mumetoweka baada ya kuchomkea hoja zenu mfu ambazo huwa hamuwezi kuzijadili baada ya copy paste....hehehe
 
Leta picha
Hio.
JamiiForums-961221674.jpg
 
Ulichomekea yale huwa mnakaririshwa Lumumba kisha ukatoweka, rudi uone jamaa wameachia nondo za uhakika uzi unachezea kurasa kadhaa sasa, Mataga wote mumetoweka baada ya kuchomkea hoja zenu mfu ambazo huwa hamuwezi kuzijadili baada ya copy paste....hehehe

Lumumba ndio wapi!! na wewe unapafahamu au unaimba tu ukisikia watu wanaimba?

kasome hoja zangu, ndio utajua hao wengine wamezielewa,kilichobaki ni kelele tu.au ubishe hazina ukweli.
 
Kama bado una mchecheto wa maandamano nenda kaungane na Bob wine
Unajua kusoma au umecomment hivi kwa sababu mtu akiwa ni mwanachama wa CCM ni lazima awe goigoi?Wapi nimezungumzia mambo ya maandamano katika comment yangu?
 
Naweza kusema Kenya bado sana kujipongeza, hadi zipite chaguzi kama tatu au nne hivi. Nasema hivyo kwa sababu, msingi wa vurugu za kisiasa Kenya ni Ukabila. Ni kweli kuna hatua fulani chanya mmepiga, lakini tatizo la ukabila bado lipo na lina nafasi ya kusababisha machafuko hasa kipindi cha uchaguzi wa Rais. Kama huamini haya maoni yangu tusubiri 2022 especially kama Raila hatagombea na kushinda.
 
Huyo mkenya anakua na akili za mbuni anaficha kichwa kwenye shimo huku wezere lipo nje.... Kenya bado hamna kitu sema wanajifariji tu
 
Back
Top Bottom