MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
- Thread starter
- #21
Naweza kusema Kenya bado sana kujipongeza, hadi zipite chaguzi kama tatu au nne hivi. Nasema hivyo kwa sababu, msingi wa vurugu za kisiasa Kenya ni Ukabila. Ni kweli kuna hatua fulani chanya mmepiga, lakini tatizo la ukabila bado lipo na lina nafasi ya kusababisha machafuko hasa kipindi cha uchaguzi wa Rais. Kama huamini haya maoni yangu tusubiri 2022 especially kama Raila hatagombea na kushinda.
Ndio maana nimesema tulioishi enzi zile, tukilinganisha na leo, tumepiga hatua pakubwa sana na nchi leo hii ni bora mara 100 ya ilivyokua, enzi hizo tulikua kwenye kiza kama ilivyo Tanzania na majirani wengine leo, rais alikua ndiye kila kitu, chochote alichokisema kilisujudiwa, aliimbiwa misifa, wananchi waliishi kwa uwoga, yaani usikike unamsema vibaya inakula kwako.
Tulifikia hatua tukachoka, tukaamua kuboresha nchi, tukachezea virungu, wenzetu wengi waliaga dunia, wengine wakalemazwa, baadhi yetu tuna makovu ila tukaishia kuvuna matunda mazuri.
Nakiri hatujafika, na hamna taifa dunia lililofika, ni mapambano ya kila siku.
Suala la ukabila hayo ni maamuzi ya watu kibinafsi, hawajalazimishwa na yeyote au serikali, mtu anaamua apige kura kwa kuzingatia ukabila, huo ni uhuru wake, kimsingi amepewa uhuru wa maamuzi, halazimishwi. Lakini kwenu huko tuliona kipindi cha uchaguzi, rais anatolea mikwara kwa Kisukuma kwamba mtu wake asipochaguliwa, basi hao wa huko wasubiri kitakachowakuta, nchi yote mumelazimishwa mapambio ya CCM, hamna uhuru, kwenu huko hata ni vigumu kuelewa tatizo lenu nini haswa, maana mna uchama, ukanda, chembe chembe za ukabila, udini n.k. ikiwemo pia hata ubaguzi dhidi ya zeruzeru, kuna wakati huwa mnaingiwa na mzuka wa kuwachinja.