Waganda wamechoka, wameingia barabarani, walikua wanatucheka enzi zetu za mapambano, haya wapambane


Ndio maana nimesema tulioishi enzi zile, tukilinganisha na leo, tumepiga hatua pakubwa sana na nchi leo hii ni bora mara 100 ya ilivyokua, enzi hizo tulikua kwenye kiza kama ilivyo Tanzania na majirani wengine leo, rais alikua ndiye kila kitu, chochote alichokisema kilisujudiwa, aliimbiwa misifa, wananchi waliishi kwa uwoga, yaani usikike unamsema vibaya inakula kwako.

Tulifikia hatua tukachoka, tukaamua kuboresha nchi, tukachezea virungu, wenzetu wengi waliaga dunia, wengine wakalemazwa, baadhi yetu tuna makovu ila tukaishia kuvuna matunda mazuri.
Nakiri hatujafika, na hamna taifa dunia lililofika, ni mapambano ya kila siku.

Suala la ukabila hayo ni maamuzi ya watu kibinafsi, hawajalazimishwa na yeyote au serikali, mtu anaamua apige kura kwa kuzingatia ukabila, huo ni uhuru wake, kimsingi amepewa uhuru wa maamuzi, halazimishwi. Lakini kwenu huko tuliona kipindi cha uchaguzi, rais anatolea mikwara kwa Kisukuma kwamba mtu wake asipochaguliwa, basi hao wa huko wasubiri kitakachowakuta, nchi yote mumelazimishwa mapambio ya CCM, hamna uhuru, kwenu huko hata ni vigumu kuelewa tatizo lenu nini haswa, maana mna uchama, ukanda, chembe chembe za ukabila, udini n.k. ikiwemo pia hata ubaguzi dhidi ya zeruzeru, kuna wakati huwa mnaingiwa na mzuka wa kuwachinja.
 
Tanzania hatujawai kua kama enzi zenu za Moi hizo roho zenu nyeusi mnazo kitambo huku hatujawahi fikia hizo level kabisa
 
Reactions: nao

Hahaaa, naona unajitahidi kuunga unga na kuokoteza vihoja ili kulazimisha fikra zako zikubalike. Lakini ukweli unaujua hata ukijaribu kuukwepa. Umezungumzia election violence huko Uganda. Ukasema Kenya imeshapita huko. Nikakuambia hapana, jipeni muda -- ukabila ndio tatizo la msingi kwenye siasa za Kenya -- kama hutaki kukubali acha tuone yajayo 2022. Mungu akipenda tukiwepo tutaona ukomavu wenu. Tanzania imevuka salama, nchi ni shwari kabisa kama kawaida yetu.
 

Jifunze kusoma na kuelewa hoja, hamna sehemu nimeongea kuhusu "post election violence" Uganda, au unatumia maneno hata bila kujua maana yake. Itakubidi uboreshe upeo wako wa uelewa ili kujadili hoja kama hizi.
 
Jifunze kusoma na kuelewa hoja, hamna sehemu nimeongea kuhusu "post election violence" Uganda, au unatumia maneno hata bila kujua maana yake. Itakubidi uboreshe upeo wako wa uelewa ili kujadili hoja kama hizi.
Mzee naona unakula za uso,
Wazee wa bbi na wheelbarrow madness,
Uchaguzi 2022 kampeni zimeanza tangu 2018,
Kila uchaguzi lazima polisi waue si chini ya raia 100 kwa risasi za Moto
Nchi ya Kizandiki sana Kenya.
 
Baada ya Lisu kupiga spana za kutosha, wakaona wajibu kwa AK-47. Baada ya uchafuzi wa uchaguzi, ameamua kwenda kukaba kwenye kiungo cha juu kule misaada inapotokea.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hii habar ni fake mk 254 ,ajaitaja tz [emoji2][emoji2]Mungu kweli ana maajabu
 
Somo la fasihi lilikupita, au ulisinzia kwenye kipindi chake.
Ayo masomo sijasoma,kwa iyo fasihi ndo imekubadilisha? Bravo kwa fasihi idumu milele[emoji41][emoji41]
 
M7 ana chake tena pale uganda. Akafuge ng'ombe zake tu kijijini
 
Sema mabadiliko mliyopigania bado hayajazaa matunda, maana wanasiasa na polisi wanawaendesha kweli. Majuzi tu kipindi cha Corona imepamba moto, mmepigwa virungu na wengine kuuawa.
 
Mbona mnapiga tena kura kubadilisha hiyo katiba?
 
Mbona mnapiga tena kura kubadilisha hiyo katiba?

Kwa sababu uhuru huo tunao, uthubutu tunao, uwezo wa kutumia ubongo tunao, uwezo wa kukubali kutokubaliana tunao......
Katiba mpya ambayo tunayo ni bora kuliko zote ukanda huu maana iliandikwa upya na wazawa wazalendo, ila kama nyaraka zoyote zingine zilizoandikwa na binadamu, inayo kasoro na hamna siku tuliafikia kwamba haitokuja ibadilishwe na kuboreshwa zaidi, kimsingi ni kuhakikisha kila badiliko humo linakubaliwa na Wakenya wote kwa maslahi ya Wakenya.

Nyie huko mumeganda na kile mlichoachiwa na mkoloni, mlijaribu kubadilisha mkaangukia pua, imesababisha uchaguzi unafanyika kwenu mithili ya usanii mtupu, mnasindika na kufuta upinzani na haikuishia hapo mkaanza kuwasaka kama nguruwe pori, wengine wamekimbilia kuja Kenya, wengine Ulaya, wengine wameuawa huko au kulemazwa hadi mabeberu wameanza wameng'aka, mkae msubiri kibano chao, wameanza kufukua namna mliwapiga hela yao ya corona.
 
Usiwafananishe Wakenya wanaojitambua na wasio waoga na Watz waliokuzwa katika mazingira ya woga...mbaya zaidi Serikali na Dola nayo inawanyanyasa wananchi

Wakenya katika kudai haki yao wapo very active nakumbuka migomo ya watumishi wa umma huko yaani Madaktari na Waalimu kudai nyongeza ya mishahara
 
Hujielewi watanzania night watu tunaojielewa kuliko nchi yoyote afrika mashariki. Ndo maana hatuandamani Kwa sababu tunajua magufuli ameshinda kihalali na ni rais mzuri na ni mtu sahihi.
hahaahahah watanzania wanajielewa tangu lini? acha kuchekesha mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…