Kwa kile kinachoonekana kuwa hali imekuwa tete nchini Uganda, baada ya mchakato kwa kubadili vifungu vya katiba vitakavyomwezesha Rais Mu7 kuwa na nafasi zaidi ya kugombea Urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao. Baada ya tetesi kwamba huenda Mu7 anaogopa kushtakiwa mahakamani kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu baada ya kutoka madarakani, Waganda walipendekeza kwamba kiwekwe kifungu katika katiba kitakacho mlinda pindi atakapo achia madaraka, lakini inaonekana juhudi hizo hazizai matunda kwani mchakato unaendelea kwa kasi kubwa.
Katika hatua ya kushangaza, limeibuka kundi linalofanya kampeni zake kumtaka Mu7 amrithishe kiti hicho mwanaye Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mshauri wake katika masuala ya uongozi. Kikundi hicho kimetohoa kifungu cha Biblia kutoka Yn 3:16 na kusema “Kwa maana jinsi hii Mu7 aliipenda Uganda, hata akamtoa mwanaye kuwa Rais wa Uganda”, wakitarajia kuwa juhudi hizo labda zitafanikiwa kumweka benchi Mu7 na kumpata Rais mpya, kijana, lakini akiwa ni mwanaye.
Sisi Watanzania tumpongeze sana Rais Magufuli (The President Incumbent) kwa kuonesha nia wazi wazi kwamba atatawala kwa mujibu wa katiba ya JMT. Ni suala la kujivunia kuwa na viongozi wa namna hii, kwani tunaona nchi nyingi zinazotuzunguka Marais wao wanavyokuwa ving’ang’anizi. Pia tuna kila sababu ya kuwapongeza Marais wetu wote waliostaafu kwa kuridhia kwa moyo mmoja na kwa amani kabisa kuachia madaraka pale muda wa uongozi wao ulipokoma. Tuiombee nchi yetu, Tudumishe amani yetu.
Benmpo