Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Leo ukiwa unaimba kwaya unarukaruka unawatukana waganga wa kienyeji na kusahau kuwa huenda sasa ungekuwa unaitwa marehemu. Ila waganga wa kienyeji ndio waliokutoa kwenye mikono ya adui zako kipindi ukiwa mtoto au kijana.
Nakumbuka nikiwa darasa la tatu siku moja nikiwa shule nilipata stroke ya miguu na ghafla nikawa Kiwete.
Nikafuatwa kwa baiskeli nikarudishwa home.
Nikawa mtu wa kukaa ndani tu, siumwi mahali popote ila miguu siwezi kuinyakua.
Siku moja nikawa najadiliana na mdogo wangu ambaye ni rika moja na mimi. Baba mmoja kasoro mama tu. Nikamwambia twende kwa mganga wa kienyeji mtaa wa pili. Nilijua nitakwenda kwa msaada wa mtu. Ile nainuka tu nikawa mzima, nilitembea mpaka kwa mganga.
Akapiga ramli bure, akanitibu bure. Nikapona moja kwa moja. Nikarudi shule nikaendelea kufanya vizuri na sasa nimegraduate shahada yangu ya kwanza ya International Relations & Diplomacy na sasa nimekuwa mlinzi mwenye degree.
Sijawahi kwenda kwa waganga miaka hii ila jana usiku nimekumbuka fadhila za yule mganga, nawaza nikampe zawadi (sio kupata huduma).
Ni miaka karibu 20 sasa sijamuona machoni. Nimewauliza kijijini wanasema bado yupo. Kumtibu mtu bure kwa tatizo kubwa kiasi kile ni upendo wa ajabu sana, hawa wachungaji wakikuponya sikio tu watakurusha kwenye tv kila siku ili kuvutia watu kwao.