Waganga wa kienyeji wametusaidia. Tusiwabeze

Waganga wa kienyeji wametusaidia. Tusiwabeze

Wanachapwa viboko vya upako wanashangilia
Mkuu Ivi ramli inakuaje ?
IMG_20201201_160822_891_1607206068619.jpg
 
Kitu ambacho hatukijui ni kuwa waganga wote wapiga Ramli ni wachawi

Vitu ambavyo hufanya ni kukuloga ili uende kwake akutibie
Ukijua hili hutasumbuka nao
 
Leo ukiwa unaimba kwaya unarukaruka unawatukana waganga wa kienyeji na kusahau kuwa huenda sasa ungekuwa unaitwa marehemu. Ila waganga wa kienyeji ndio waliokutoa kwenye mikono ya adui zako kipindi ukiwa mtoto au kijana.

Nakumbuka nikiwa darasa la tatu siku moja nikiwa shule nilipata stroke ya miguu na ghafla nikawa Kiwete.

Nikafuatwa kwa baiskeli nikarudishwa home.

Nikawa mtu wa kukaa ndani tu, siumwi mahali popote ila miguu siwezi kuinyakua.

Siku moja nikawa najadiliana na mdogo wangu ambaye ni rika moja na mimi. Baba mmoja kasoro mama tu. Nikamwambia twende kwa mganga wa kienyeji mtaa wa pili. Nilijua nitakwenda kwa msaada wa mtu. Ile nainuka tu nikawa mzima, nilitembea mpaka kwa mganga.

Akapiga ramli bure, akanitibu bure. Nikapona moja kwa moja. Nikarudi shule nikaendelea kufanya vizuri na sasa nimegraduate shahada yangu ya kwanza ya International Relations & Diplomacy na sasa nimekuwa mlinzi mwenye degree.

Sijawahi kwenda kwa waganga miaka hii ila jana usiku nimekumbuka fadhila za yule mganga, nawaza nikampe zawadi (sio kupata huduma).

Ni miaka karibu 20 sasa sijamuona machoni. Nimewauliza kijijini wanasema bado yupo. Kumtibu mtu bure kwa tatizo kubwa kiasi kile ni upendo wa ajabu sana, hawa wachungaji wakikuponya sikio tu watakurusha kwenye tv kila siku ili kuvutia watu kwao.
picha
 
Sasa mbona unasema mganga ndio anakuroga ili uwende kwake akutibu?
Nilichokuambia ni kweli wewe jidai kakuloga mwingine uende kwa mwingine hapo wanashindana wao kwa wao atakayezidiwa anapelekwa kifungoni

Namaanisha waganga wako wengi akikuloga mmoja harafu wewe ukaenda kwa mganga mwingine umewachangonganisha wanaanza kupimana wao wenyewe sasa

Labda huyo uliyeenda kwake awe mzito

Lkn na wachawi ambao siyo waganga pia wapo jua hivo
 
Nilichokuambia ni kweli wewe jidai kakuloga mwingine uende kwa mwingine hapo wanashindana wao kwa wao atakayezidiwa anapelekwa kifungoni

Namaanisha waganga wako wengi akikuloga mmoja harafu wewe ukaenda kwa mganga mwingine umewachangonganisha wanaanza kupimana wao wenyewe sasa

Labda huyo uliyeenda kwake awe mzito

Lkn na wachawi ambao siyo waganga pia wapo jua hivo
Sasa mkuu utajuaje kuwa tatizo ulilonalo ni uchawi na aliyekuroga ni mganga fulani ili uende kwa huyo mganga aliyekuroga? Mimi sidhani kama unachosema kina uhalisia,mfano eneo naloishi hakuna mganga ila kuna watu wanaohisiwa ni wachawi tu hawatibu mtu wao wanahisiwa kuwaroga watu basi,sasa mfano nikijiona nimerogwa ndio nitasema niende kwa hao wachawi ili wanitibu au kutakuwa na mganga huko kwengine kabisa na eneo langu ndio kaniroga?
 
Mtoto alitaka kumchukua msukule baba yake, baba alishtuka akaenda kwa mganga na akaambiwa imebaki wiki tu aondoke duniani. Mganga akamgeuzia kibao Yule mtoto akafa kwa ajali ya bajaji. Baba akapona na akasema kaburi la mwanae liongezewe m moja kwenda chini. Mganga kamuokoa mzee!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Nipe connection mkuu.
 
Back
Top Bottom