Waganga wa Kinyeji Simiyu Tumechoka na michango ya Mwenge

Waganga wa Kinyeji Simiyu Tumechoka na michango ya Mwenge

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245
Ndugu wana jukwaa, Leo naomba nilete hii hoja kwenu.

Sisi waganga wa Tiba asili au waganga wa Kinyeji Mkoa wa Simiyu, tumechoka na michango ya lazima Kwa ajili ya Mwenge.

Kila Mwaka tumekuwa tunachangishwa tena Kwa lazima, usipochanga unawekewa vikwazo na vitisho kibao.

Kila Mwaka tunachangishwa, kwanini serikali isiwekee bajeti Mwenge, Kwa Nini watu tuchangishwe? Tena Kwa lazima?

Tumechoka kuchangishwa hela za mwenge kila mwaka. Lakini mashekhe na wachungaji wao wanaachwa wakati wote tunatoa huduma sawa kwenye jamii.

Serikali iwe inautengea mwenge bajeti yake.
 
Sio nyie tu mkuu. walimu hasa wa shule za msingi za serikali wanachanga kwa lazima, kwa kuambiwa serikali imewapa dhanama hivyo ni lazima wachangie
 
Kama Mganga Kweli Mloge Samuya
Watanganyika wengi hatumpendi.

Mganga Unalalamika!!!!
Unalia!!!!!!!
 
Si muwaroge au uganga wenu wa uongo..!!
Halafu nyie ndo mnaotuma watu viungo vya albino muongezewe tozo mpaka za kupumua..!!
Nyie mnachangia sana mauaji ya raia..
 
Uchangishaji wa pesa ya mwenge ni upigaji kwa sababu bajeti yake huwa ipo michango hutolewa risiti ya mkono na siyo EFD.
 
Ndugu wana jukwaa, Leo naomba nilete hii hoja kwenu.

Sisi waganga wa Tiba asili au waganga wa Kinyeji Mkoa wa Simiyu, tumechoka na michango ya lazima Kwa ajili ya Mwenge.

Kila Mwaka tumekuwa tunachangishwa tena Kwa lazima, usipochanga unawekewa vikwazo na vitisho kibao.

Kila Mwaka tunachangishwa, kwanini serikali isiwekee bajeti Mwenge, Kwa Nini watu tuchangishwe? Tena Kwa lazima?

Tumechoka kuchangishwa hela za mwenge kila mwaka. Lakini mashekhe na wachungaji wao wanaachwa wakati wote tunatoa huduma sawa kwenye jamii.

Serikali iwe inautengea mwenge bajeti yake.
Tambiko la Mwenge lilihusisha watu wote bila kujali mila,dini, tamaduni,itikadi,uganga, ulozi na Kanisa Takatifu hivyo basi iweje wewe ulalamikie kuchangia sh2000 ya mwenge
 
Back
Top Bottom