Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Ni historia inayojirudia ambapo mkoloni ni kama ameona njia ya kuwapumbaza Waafrika na kuwatawala kiurahisi ni kuwataka wapigane wenyewe, waonane wabaya wao kwa wao.
Nchi ya DRC inakadiriwa kuwa na vikosi vya uhalifu zaidi ya 100 je tuseme vikosi hivi vyote vinadhaminiwa na Rwanda?..Inasemekana kuna mpaka viwanja bubu vya ndege misituni navyo tuseme ni Rwanda kupitia Rais Paul Kagame ndiye anayevijenga?.
Tafiti zinaonesha kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ina mtandao mkubwa wa viwanja vya ndege, vingi vikiwa katika maeneo ya misitu na vijijini. Hata hivyo, idadi kamili ya viwanja vya ndege vilivyoko porini haipatikani kwa urahisi kutokana na ukubwa wa nchi na ukosefu wa takwimu za kina. Usafiri wa anga ni muhimu nchini DRC kwa sababu ya changamoto za miundombinu ya barabara, hasa katika maeneo ya misitu. Hata hivyo, sekta ya usafiri wa anga nchini humo inakabiliwa na changamoto za usalama kutokana na miundombinu duni na usimamizi dhaifu.
Afrika inagawanywa ili itawalike, tunaoneshewa kivuli cha adui ila siyo adui halisi. Leo ni kama tunaaminishwa machafuko yote ya nchi ya Jamhuri ya Kongo kiini ni Rwanda. Tunapandikiziwa imani fulani ya kuchukiana sisi kwa sisi na wengine tunatumiwa vibaya kwa maslahi ya mabeberu. Afrika inatumiwa yenyewe kujimaliza.
Ipo haja ya kutafuta sababu chanzi na kuacha kutafuta sadaka ya kafara kwa maslahi ya wakubwa. Uhakika ni kuwa raslimali za DRC zimewekewa mirija ya wakubwa na utete wa usalama ni kwa maslahi yao na siyo ya Afrika na kwa upekee Afrika Mashariki.
Inaonekana kinachotafutwa sasa siyo kusababisha hali tete katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki ili wachote raslimali vizuri. Ikumbukwe wanachokifanya leo ni mpango wa muda mrefu na hawabahatishi.
Mungu awape hekima Marais, wa nchi zote za Afrika na kwa upekee ukanda huu wa Afrika Mashariki.