Wageni Wako Wananuka?...

Wageni Wako Wananuka?...

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Katika website ya waynesthisandthat nimepata quote hii ambayo kwangu mimi hai'saund vizuri sana;

.."Like Fish, Guests Begin Smelling After Three Days"...!

Lakini pia, kwa waliosoma vitabu vya zamani primary, kuna habari ya mgeni isemayo:

Mgeni siku ya kwanza,
Mpe mchele na panza,
Mtilie kifuuni ,
Mkaribishe mgeni,

Mgeni siku ya pili
Pika wali kwa samli...(nimesahau linaishaje).

Lakini, ubeti wa nne(ambapo ni siku ya nne ya mgeni) unasema hivi:

Mgeni siku ya nne,
Mpe jembe akalime,
Akirudi muagane ,
Aende zake mgeni.

Wadau, mmegundua lolote kwa wageni wenu majumbani wakaapo siku 3 na kuanza ya 4?
 
Kwa kweli wageni wakitanzania ukiwaendekeza utafulia huku unaona...Ni vyema ukawa na principles katika nyumba yako na kila mtu lazima azifuate.kwa mfano mimi nyumbani kwangu nimeweka ratiba ya chakula ya wiki nzima,wenyewe tunajua kwa kila siku tunakula nini.Utakuta mgeni anakuja kwako na kujifanya eti hali ugali na dagaa,lol anataka umbadilishie,ukibadilisha siku nyingine tena kelele zinaanza...Mimi they have to obey with my principles mtu ambaye ninaweza kumsikiliza ni yule ambaye labda ana allergy au mtoto basi,wengine twende kazini kama hawezi basi ajihudumie kwa uwezo wake.
 
Mimi they have to obey with my principles mtu ambaye ninaweza kumsikiliza ni yule ambaye labda ana allergy au mtoto basi,wengine twende kazini kama hawezi basi ajihudumie kwa uwezo wake.
Mkuu,
do, wewe nadhani umedhibiti haya mambo!
Lakini hii sifa ya ukarimu wa watanzania huoni unai'defy?
 
Mkuu,
do, wewe nadhani umedhibiti haya mambo!
Lakini hii sifa ya ukarimu wa watanzania huoni unai'defy?

Ukarimu ni sawa lakini isiwe yule anayekarimiwa anaanza kuchagua chakula as if anajua mfuko wako upoje! Sote kwa namna moja ma nyingine tumewahikuwa wageni wa wengine (au siku moja tutakuwa wageni). Ukiwa ugenini si vema kuanza kudictate mambo kwenye nyumba ya watu kama vile upo kwako.

Kuna wageni wanakera bwana, siku mbili tu utatamani endezake!
 
mie kwangu,mgeni kama ni mstaarabu(asiniwekee masharti) atakula kilichopo,lakini akileta nyodo ni cassava tu kwa kwenda mbele hadi siku ya kuondoka
 
mie kwangu,mgeni kama ni mstaarabu(asiniwekee masharti) atakula kilichopo, lakini akileta nyodo ni cassava tu kwa kwenda mbele hadi siku ya kuondoka

😡😡
Mkuu unatisha!
 
ooops kuna wageni wengine ukipika hiki hatumii,ukifanya hivi hapendi mradi anakuwekea masharti ndani ya nyumba yako mwenyewe ..pazuri hapo ...
 
Mambo mengi yanaturudisha nyuma kimandeleo,likiwemo la wageni, lakini kwa kweli huwezi kuavoidi inabidi ukubali matokeo,utawafukuza?Ebu fikiria, watu 20 wamekuja kwenye HARUSI na baada ya hapo hawatoki hadi........baadae sana.
 
Lakini mbona kuna msemo kwamba mgeni ndani ni BARAKA?
Hii nayo ikoje?
 
Mgeni halisi anajua yake asili
Mgeni asiyeambilika kwangu siku mbili
Mgeni kwangu heshima mara mbili
Chakula atakula hata kama pilipili

Mgeni mateso kwako wa kazi gani
Mgeni furaha na sio huzuni
Mgeni amani na sio majonzini
 
PJ mgeni ni baraka ndio, maana kuna nyumba hazitembelewi na wageni but maisha ya sasa tofauti na zamani mfano sasa kuna swala la usafiri(nauli)chakula kimepanda mfano zamani unachuma tembele,mchicha kisamvu etc hapo nyumbani ,but nowdaiz tembele chana moja 200,then lazima tukubaliane na hili wageni hasa wa mkoa wanakula sana hii ni kutokana na mazingira,ebu fikiria mfano mgeni anakuja kwako kaja labda kwenye semina,hakwambii ni ya muda gani,pili kila asb anakuomba nauli!utajiskiaje?maisha magum soseji ni za mtoto xul mgeni anataka apikiwe,matunda yamepanda bei juic unatengeneza ya mtoto tu mgeni anakunywa utasema kuna baraka au nuksi hapa?then bado akiondoka anataka uumpe nauli na zawadi za kupeleka hme kwao,akila mezani hata chombo hatoi kisa mgeni!lazima tuwe wawazi maana hela yenyewe kushnehi,budget inabana,mgeni aje sawa lakini gharam ndogo ndogo achangie jamani.Hata mm nikienda kwake ntachangia maramoja moja na kilo ya nyama,sukari etc
Lakini mbona kuna msemo kwamba mgeni ndani ni BARAKA?
Hii nayo ikoje?
 
ooops kuna wageni wengine ukipika hiki hatumii,ukifanya hivi hapendi mradi anakuwekea masharti ndani ya nyumba yako mwenyewe ..pazuri hapo ...

Hao watanifanya niwe na attitude mbaya sana aisee. Kwenye msosi nitaelewa kwa sababi si watu wote hula vyakula vyote. Lakini tunapoanza kuwekeana masharti...ooh no...nitakutimua.
 
ooops kuna wageni wengine ukipika hiki hatumii,ukifanya hivi hapendi mradi anakuwekea masharti ndani ya nyumba yako mwenyewe ..pazuri hapo ...

mbaya zaidi awe ni wifi au shemeji, ukifanya kinyume na anvotaka akitoka hapo ujue ukweni utaeleweka vibaya.
 
Hao watanifanya niwe na attitude mbaya sana aisee. Kwenye msosi nitaelewa kwa sababi si watu wote hula vyakula vyote. Lakini tunapoanza kuwekeana masharti...ooh no...nitakutimua.

hujaniwekea masharti nuymbani kwangu bado loh!! utachapa mwendo ASAP!!!
SHEMEJI TENA UKIJA KWANGU KEEP THIS IN MIND!!!
 
hujaniwekea masharti nuymbani kwangu bado loh!! utachapa mwendo ASAP!!!
SHEMEJI TENA UKIJA KWANGU KEEP THIS IN MIND!!!

Hey shem...how was your weekend? I thought about you and wanted to call you but I decided not to....

Shem kwako ni kwangu na kwangu ni kwako.....
 
Hey shem...how was your weekend? I thought about you and wanted to call you but I decided not to....

Shem kwako ni kwangu na kwangu ni kwako.....
Shem si unajua nauguza, wikend yetu haikiwa njema sana lakini leo hatujambo.

ni sawa shem lakini kuwe na mipaka angalau jamani maana sasa ntatofautishaje wewe na Bala!!!
 
Hey shem...how was your weekend? I thought about you and wanted to call you but I decided not to....

Shem kwako ni kwangu na kwangu ni kwako.....
EEH!i am still in vain!cant connect'em dots lolz!
 
Back
Top Bottom