Katika website ya waynesthisandthat nimepata quote hii ambayo kwangu mimi hai'saund vizuri sana;
.."Like Fish, Guests Begin Smelling After Three Days"...!
Lakini pia, kwa waliosoma vitabu vya zamani primary, kuna habari ya mgeni isemayo:
Mgeni siku ya kwanza,
Mpe mchele na panza,
Mtilie kifuuni ,
Mkaribishe mgeni,
Mgeni siku ya pili
Pika wali kwa samli
Na nyama ratili mbili
Kaa ule na mgeni
Mgeni siku ya tatu
Nyumbani hamna kitu
Muna vibaba vitatu
Pika ule na mgeni
Lakini, ubeti wa nne(ambapo ni siku ya nne ya mgeni) unasema hivi:
Mgeni siku ya nne,
Mpe jembe akalime,
Akirudi muagane ,
Aende zake mgeni.
Mgeni siku ya tano
Mwembamba kama sindano
Hakuishi minong'ono
Asemwa yeye mgeni
Mgeni siku ya sita
Mkila mnajificha
Nani akimbiwaye
Akimbiwae mgeni
Mgeni siku ya saba
Si mgeni ana baa (hii nimesahau...)
Mgeni siku ya kumi
Kwa mateke na magumi
Nani afukuzwaye
Afukuzwa ye mgeni
Wadau, mmegundua lolote kwa wageni wenu majumbani wakaapo siku 3 na kuanza ya 4?