Wageni Wavamia Biashara Kariakoo Bila Vibali, Mamlaka Zatazamana

Wageni Wavamia Biashara Kariakoo Bila Vibali, Mamlaka Zatazamana

Majitha

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
25
Reaction score
14
Katika hali inayoibua maswali mengi kuhusu uzingatiaji wa sheria na maslahi ya taifa, maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam yameendelea kushuhudia wimbi la wageni wanaojihusisha na biashara bila kuwa na vibali halali, huku mamlaka husika zikituhumiwa kufumbia macho au hata kuhusika moja kwa moja na ukiukwaji huo wa sheria.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa wafanyabiashara hao wa kigeni, wengi wao wakiwa kutoka nchi za Asia wamejipenyeza katika mifumo ya biashara ya jumla na rejareja, wakimiliki maduka, maghala, na hata kufanya usambazaji wa bidhaa bila kuwa na vibali vya kazi, ukaazi au leseni za biashara.

Hali hiyo imezua taharuki kwa wafanyabiashara wazawa ambao wanalalamikia ushindani usio wa haki, kuporomoka kwa bei za bidhaa, na kupungua kwa mapato yao huku wakilazimika kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kulipa kodi na ada mbalimbali.

“Tunafanya biashara kwa hasara kwa sababu hawa wageni wanauza bidhaa kwa bei ya chini kupita kiasi, hatujui wanazitoa wapi wala kama wanalipa kodi. Tukienda TRA au Manispaa, hakuna hatua yoyote inachukuliwa,” alisema mmoja wa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.

Taarifa kutoka ndani ya baadhi ya taasisi za udhibiti zinaeleza kwamba upungufu wa usimamizi, udhaifu wa mifumo ya ufuatiliaji, na matukio ya wazi ya rushwa vimechangia hali hiyo kuendelea kushamiri kwa kasi kubwa.

Msemaji mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema, “TRA inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha wafanyabiashara wote wanasajiliwa na wanalipa kodi stahiki. Tukigundua ukiukwaji, tunachukua hatua stahiki.”

Hata hivyo, hali halisi mtaani inaonyesha kuwa hatua hizo hazitoshi. Wageni wengi wanaonekana wakifanya shughuli za moja kwa moja za rejareja, baadhi hata kuuza bidhaa mtaani au kuendesha maduka kwa majina ya wenyeji huku wao wakiwa wamiliki wa kweli – kinachoashiria uwepo wa mtandao mpana wa ushirikiano wa kifisadi baina ya baadhi ya wenyeji na wageni.

Wadadisi wa masuala ya kiuchumi na sera wanatahadharisha kuwa endapo hali hii itaachwa iendelee, uchumi wa ndani utadhoofika, mapato ya serikali yatapungua, na zaidi, inaweza kuchochea migogoro ya kijamii kutokana na chuki zinazojengeka dhidi ya wageni.

“Hii ni bomu linalosubiri kulipuka. Ni wakati sasa kwa mamlaka kuchukua hatua za kweli, si za kuigiza. Ulinzi wa maslahi ya taifa ni kipaumbele cha kila taasisi ya umma,” alisema mchambuzi wa sera kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Biashara inapaswa kuandaa operesheni kabambe ya kuhakiki vibali vya kazi na biashara kwa wageni, kuhakikisha sheria zinasimamiwa kwa haki na bila upendeleo, sambamba na kuwachukulia hatua kali wale wote – raia au wageni – wanaoshiriki katika biashara haramu.

Kwa sasa, macho ya wananchi na wadau wa biashara yanaitazama serikali kwa matumaini na mashaka, ikisubiri kuona kama itathibitisha dhamira ya kweli ya kulinda maslahi ya taifa au itaendelea kuwa kimya huku wageni wakitawala uchumi wa Kariakoo kwa njia zisizo halali.

Naondoka huku nikiweweseka, langu jina ni Sendi Muwanga,
Aufwiedersehen.
 
Hali hiyo imezua taharuki kwa wafanyabiashara wazawa ambao wanalalamikia ushindani usio wa haki, kuporomoka kwa bei za bidhaa, na kupungua kwa mapato yao huku wakilazimika kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kulipa kodi na ada mbalimbali.

“Tunafanya biashara kwa hasara kwa sababu hawa wageni wanauza bidhaa kwa bei ya chini kupita kiasi, hatujui wanazitoa wapi wala kama wanalipa kodi. Tukienda TRA au Manispaa, hakuna hatua yoyote inachukuliwa,” alisema mmoja wa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.
Mawinga wa Kariakoo mnaweweseka. Tangu boya mmoja mzawa atake kunipiga 45K kwa kipafyumu fulani hivi, kuzunguka kwa Mchina kipafyumu kile kile kumbe kinauzwa 15K sina hamu na mawinga aisee. Tunaomba ushindani huu uendelee ili bei zizidi kushuka kwa wateja. Labda itasaidia kwa hawa mawinga wazawa kupunguza upigaji kwa kupandisha bei kiholela.

Tena Ubungo complex inayojengwa na Wachina ikamilike mapema tuone kama itasaidia kushusha bei.

Competition is good to the consumer; and as far as I am concerned, that's all what matters to me!
 
Sababu wasukuma mna bei zenu sio kosa la winga….! 😹😹
 
Sababu wasukuma mna bei zenu sio kosa la winga….! 😹😹
Siyo poa hata kama ni Msukuma!

Halafu kuna mahali nilikutag hukutokea. Nikajua uko bize na maokoto kama kawaida yako!

Screenshot_20230602_173056_Chrome.jpg
 
Watanzania wenyewe ndiyo wapuuzi, hao wageni huwa wanawatanguliza mbele Wabongo kufanikisha ujanja wao kwa vipesa vidogo tu.
 
Shida ni mfumo mbovu wa serikali na CCM.
Bado mjasema kila sekta itashikwa makende
 
Back
Top Bottom