Hii kwako mr
Da'Vinci na kwa wengine wenye mitazamo eti wamisri walikuwa weusi tii. sijui ni misingi gani mnabase your claim. Nadhani mnatumia misingi ya ubara na urangi, eti kwa kuwa misri ipo pamoja na bara la Afrika, eti kama njia ya kuonyeaha mtu mweusi nae yumo. Si sawa kufanya hivyo tafuta ukweli na ukweli atakuweka huru.
Mimi napinga kuwa wamisri wa kale walikuwa weusi kwa kutumia kanuni za kigeographia. Yatupasa kujua watu katika sayari yetu hapo kale walikuwa wametenganishwa kwa namna mbalimbali: kuna bahari,kuna mito, kuna mabonde ya ufa, kuna milima, na pia kuna majangwa. Hili la mwisho jangwa watu huwa hawazingatii kabisa lakini sisi waafrika rangi nyeusi twapaswa kujua the great sahara desert kama moja wapo wa ukinzani uliotukinga na maendeleo kwa miaka mingi hapo nyuma.
Ukitazama ramani yako chini ya jangwa la sahara ndio kuna watu weusi juu yake kuna watu rangi nyeupe. Ukiuliza kwa nini ni kwa sababu ilikuwa haiwezekani enzi hizo weupe kushuka chini na weusi kwenda juuu. In short wamisri wenyewe walishindwa kufwatilia chanzo cha mto nile kutokana na ukakasi uliletwa na jangwa. Imagine wamisri wangefika Victoria si wangetuabudu kama miungu wao na kutupa ujuzi wao wote. Mbali na kuwa kizuizi kikuu pia ilipelekea kusini kutokupata farasi na farasi ndio ilikuwa yaendesha uchumi kipindi hicho. Sasa tunapata taabu sana kwa sababu kuna baadhi ya stage wafrika weusi hatujapitia katika maendeleo yetu.