Ku a muda natamani tukae tupige historia za Mesopotamia, Misri, Israel,Norway, Greece, basi tu hua Napenda sana masuala ya historia na deity mbalimbali...
Ila misri kwakua ni hapahapa Afrika napenda Zaid.
wakati mfamle Themistocles wa Jiji la Athens (Ugirki) anahangaika kuhamasisha wafalme wa majiji mengine kama Queen Gogo, King Leonidas waungane wawe taifa moja wao wamisri walikua wanafanya vumbuzi kubwa kubwa zilizoacha ulimwengu kinywa wazi. Nitaorodhesha baadhi ya mambo machache ambayo yamegunduliwa na wamisri weusi kipindi hiko hata Amerika kunakaa nyani na sokwe ,Red Indian na Wamaya
Baadhi ya vitu vilivyogunduiwa na wamisri
Mathematics
Wakati wanasayansi kutoka ugiriki kama Euclid,Pythogras,Archimedes na ugiriki kwa ujumla wakipewa heshima ya kuvumbua hisabati lakini ukweli mchungu ni kwamba wamisri ndio wamegundua hisabati. Geometry,survey,vyote hvyo vimegunduliwa Misri.
Maandishi
Wamisri ndio waliogundua mfumo wa kuweka lugha yao katika maandishi, walikua na mfumo wao wa maandishi unaitwa pictograms, kutokana na picha hizo ndipo kulipozaliwa herufi mbalimbali lakini hii iliendelezwa zaidi na wagiriki’
Dawa ya meno
Kama meno yako ni meupe na masafi basi nenda katambikie kuheshimu mizimu ya mababu zenu wa kimisri maana bila wao tusingepata dawa ya meno.
Wigi, Make-Up na Vipodozi
Mnasikia kua mwanamke mzuri zaidi duniani ni Cleopatra, basi uzuri wake ulichagizwa na vipodozi na make ups za kutosha. Wewe dada waheshimu sana wamisri maana bila wao sijui ingekuaje, miaka hiyo hata Yakobo hajahamia misri..watu wa misri walikua washagundua kuvaa mawigi,kutengeneza vipodozi na kufanya make up. Wanja na kuchonga nyusi kumeanzia huko misri, mafarao ilikua sifa kwao kupaka wanja na make up..nyusi wananyoa zote. Ikumbukwe kwamba wamisri walikua hawapaki wanja kama urembo ila ilikua ni kwa ajili ya imani zao pia waliamini kufanyia macho urembo kulikua kunawasaidia kuwakinga na magonjwa ya macho.
Wino Mweusi, Karatasi na Meza
Juhudi za watu weusi ndio zinafanya wazungu waweze kukaa na kuandika propaganda zao kuhusu watu weusi.wamisri ndio wamegundua wino mweusi kwa ajili ya kuandikia na kutengeneza meza. Wakati wazungu na watu wa jamii zingine wakitumia mbao,mawe na ngozi katika kuandika Wao wamisri walivumbua Karatasi za kuandikia zilikua zinaitwa “papylus sheets”. Baadae wagiriki waliziboresha na kuziita paper kutokana na neno Papyrus.
Mashine za kuvuna na kusaga nafaka na kilimo cha umwagiliaji
Wao ndio walivumbua mashine za kuvuna na kusaga/kukoboa nafaka hasa ngano, miaka hii Israel ndio inasifika kwa kilimo cha umwagiliaji na kua sehemu ya tafiti za kilimo cha umwagiliaji duniani lakini ukweli ni kwamba misri ya kale ndio ilianza kugunda kilimo cha umwagiliaji. Wamisr wa kale walijenga mifereji mingi kusambaza maji kutoka mto nile kupeleka mashambani.
Majira na Kalenda
Wakati red Indians wa marekani wakiokota matunda nan a kuwinda wadudu kama mlo wa siku kwenye misitu mikubwa iliyokuwepo Newyork miaka ya 1300AD, Miaka karibia elfu kadhaa iliyopita kabla ya Kristo wazee wa Afrika kutoka misri walikua wameshagundua jinsi ya kutambua saa za siku na kutengeneza kalenda ya kuonyesha majira ya mwaka. Kalenda yao ilikua na miezi 12 na siku 365, kila mwezi ulikua na siku 30…lakini pia walikua washatengeneza saa zao za asili ajili ya kupima masaa ya siku.
Kufuli
Wamisri ndio watu wa kwanza kuvumbua kufuli, unambiwa funguo za kufuli zao zilikua zinauweza kua na urefu wa futi 2. Lakini hawa mababu pia sometimes kwenye IT tunawataja kama watu wa kwanza kutengeneza codes, maana ile milango ya Pyramids kuna mingine haifunguliwi na funguo ila ni codes Fulani walizoziweka miaka zaidi ya elfu 5 iliyopita. Hivyo hata coding tunaweza sema imeanzia misri.
Polisi na Serikali
Kama ulikua hujui basi ndio hivyo polisi zimeanzishwa kwa mara ya kwanza misri, polisi walikua wanatumia siraha na mbwa katika kufanya doria zao. Hakuna maskini wala tajiri aliyekua juu ya sharia halafu adhabu zao ilikua kukupa kichapo, kukuhasi,kukata pua na maskio halafu ukifa ulikua huzikwi unatupwa kama mzoga. Wamisri walikua wanaamini kwamba ukizikwa kwa heshima basi kunauwezekano mkubwa wa kwenda kwenye maisha ya baadae/mbinguni/Afterlife. Mifumo hii ya serikali zetu duniani unazoziona sasa imetengenezwa na wamisri ndio maana Yosef mtoto wa Israel alikua waziri mkuu kipindi kile. Yaani wakati Abrahm Lincoln anatunga definition ya Democracy huko misri wao walikua washamaliza kia kitu kuhusu mifumo-endeshi ya serikali (ujamaa,Udikteta,ubepari nk nk)
Egyptian Hieroglyphics (Aka Emoji za Misri😆)
View attachment 1902031
Hii ni michoro adhimu kabisa iliyobuniwa na wazee wa kiafrika ili kuwasiliana, pia zilikua zinatumika kueleza matukio yaliyopita na yajayo..so ilitumika kuweka rekodi za jamii ya watu wa misri. Unaweza kuona mchorouiliochorwa miaka zaidi ya elfu tano iliyopita ukionyesha image ya aeroplane ni ile ie iliyochorwa na Davinci miaka ya 1600sBC